TAKUKURU DODOMA YAOKOA ZAIDI YA TSH.MILIONI 135


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa[TAKUKURU] mkoa wa Dodoma imeokoa Jumla ya Tsh.Milioni 135,laki 9 ,48 elfu  na mia 193 kwa kipindi cha miezi 6.


Akizungumza na  Mtandao  Wa Mpekuzi Blog Mapema leo Agosti 13,2019  Ofisini  kwake jijini Dodoma,Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Dodoma ,Bw.Sosthenes Kibwengo amesema Fedha hizo zimeokolewa kwa kipindi cha Miezi 6 kuanzia  Mwezi Januari,hadi Juni ,2019.


Bw.Kibwengo amesema kwa kipindi cha miezi sita pia zimedhibibitiwa Jumla ya Tsh.Milioni 322,laki 3 ,48 elfu na mia 989.


Aidha,Bw.Kibwengo amebainisha kuwa katika kipindi hicho cha miezi 6 kuanzia Januari hadi Juni ,2019 TAKUKURU Mkoa wa Dodoma  imepokea jumla ya Malalamiko 231  ya vitendo vya rushwa .


Bw.Kibwengo amesema asilimia 28% ya Malalamiko hayo yanatoka Serikali za mitaa[TAMISEMI],Ardhi kwa asilimia 26.5%,Polisi 7% na mahakama   malalamiko kwa asilimia 6% na asilimia zilizobaki ni kwa sekta nyingine huku akitaja Wilaya iliyo na Malalamiko mengi ni Wilaya ya Dodoma Mjini.


Pia amesema kuanzia mwezi huu wa Agosti ,2019 wanatarajia kufungua ofisi za TAKUKURU Eneo la Chemba huku akitoa wito kwa wananchi kuwa na ushirikiano na Taasisi hiyo na kuweza kuitumia namba ya bure 113 pindi wanapoona vitendo vya rushwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527