Askofu Shoo Achaguliwa Tena Kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)

Askofu Dkt Fredrick Shoo amechaguliwa kwa kipindi kingine cha pili kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kipindi cha miaka minne.

Dkt. Shoo ametangazwa mshindi usiku wa kuamkia leo dhidi ya wagombea wengine katika uchaguzi huo ambapo ataliongoza kanisa hilo kwa kipindi kingine cha miaka minne (2019-2023). 

Askofu Shoo amepata kura 144 huku mshindani wake wa karibu, Dkt. Abednego Keshomshahara akipata kura 74 kati ya kura 218 zilizopigwa katika mzunguko wa mwisho baada ya kubaki wao wawili.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post