AJALI YA BASI NA LORI YAUA WATU WANNE,KUJERUHI 26 MOROGORO | MALUNDE 1 BLOG

Friday, August 16, 2019

AJALI YA BASI NA LORI YAUA WATU WANNE,KUJERUHI 26 MOROGORO

  Malunde       Friday, August 16, 2019
Watu 4 wamefariki dunia na wengine 26,  wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyohusha basi la abiria la Safari Njema na Lori  kugongana uso kwa uso katika eneo la Nanenane Manispaa ya Morogoro.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo imehusisha basi la abiria lenye namba za usajili T212 DNU na Lori.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa,Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi ambaye alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua taadhari.

"Ni kweli usiku wa kuamkia leo Ijumaa August 16, saa saba na nusu usiku imetokea ajali eneo la Nanenane, Morogoro, basi mali ya kampuni ya Safari Njema ambayo ilikuwa inatokea DSM kwenda Dodoma imegongana kwa ubavu na lori mali ya Tumbaku Alliance, watu 4 wamefariki.

"Ingawa watu 4 wamefariki ila abiria wengine waliokuwa kwenye basi walikimbizwa Hospitali ya Mkoa Morogoro sababu ya mshtuko na wengi wametibiwa na kuruhusiwa, wamebakia abiria 3 wanaendelea na matibabu, dereva wa lori ni miongoni mwa waliofariki.

"Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi ambaye aliovertake pasipo kuchukua tahadhari na kukutana na gari nyingine mbele kisha ajali ikatokea, dereva wa basi ametoweka na tunamtafuta, kama hatopatikana tutamkamata mmiliki wa basi ili atuoneshe dereva alipo". Amesema MutafungwaUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post