ACACIA YARUHUSIWA KUENDELEA KUSAFIRISHA DHAHABU KUTOKA MGODI WA NORTH MARA

Kampuni ya Acacia imeruhusiwa kuendelea na utaratibu wa kusafirisha dhahabu baada ya kuzuiliwa kwa takribani mwezi mmoja na Tume ya Madini Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Acacia inaeleza sasa wataanza kusafirisha madini kutoka North Mara baada ya kutimiza masharti.

Hata hivyo, Tume ya Madini imesema inaamini baadhi ya vipengele vya kanuni ya madini ya mwaka 2010 vilikiukwa na imewataka kuwasilisha mpango wa uchimbaji na ripoti ya upembuzi yakinifu ifikapo Ijumaa ya wiki hii.

Acacia imekuwa kwenye mvutano wa muda mrefu na Serikali baada ya kuzuiwa kusafirisha Makinikia nje ya nchi kwa madai ya kutolipa mrabaha stahiki.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527