TUME YA VYUO VIKUU NCHINI (TCU) YAVIFUNGULIA VYUO AMBAVYO VILIFUNGIWA KUDAHILI WANAFUNZI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 16, 2019

TUME YA VYUO VIKUU NCHINI (TCU) YAVIFUNGULIA VYUO AMBAVYO VILIFUNGIWA KUDAHILI WANAFUNZI

  Malunde       Tuesday, July 16, 2019

Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imevifungulia vyuo ambavyo vilifungiwa udahili kikiwemo Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji, Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian Bagamoyo, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), na Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Mihayo (AMUKTA).

Akizungumza wakati wa Maonyesho ya TCU yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jana Jumatatu Julai 15, 2019, Mkurugenzi wa Uratibu na Udahili wa tume hiyo, Dk Kokuberwa Katunzi-Mollel alisema vyuo hivyo vimeruhusiwa kufanya udahili baada ya kukidhi vigezo vilivyotakiwa.

Tayari dirisha  la udahili kwa mwaka huu  limefunguliwa kwa awamu ya kwanza kuanzia jana Jumatatu Julai 15 hadi Agosti 10, 2019, hivyo  akawataka wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu kuanza kutuma maombi.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post