Picha : BENKI YA TPB YATOA MSAADA WA RANGI KUPENDEZESHA SHULE YA SEKONDARI BULUBA

Benki ya TPB imetoa msaada wa rangi ndoo 50 katika shule ya Sekondari Buluba iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kupendezesha mandhari ya shule hiyo na kuiweka katika mazingira mazuri ili wanafunzi wajisomee kwa bidii na kupata ufaulu mzuri.


Msaada wa ndoo za rangi umetolewa leo Julai 18,2019 shuleni hapo na Mkurugenzi wa Masoko kutoka makao makuu ya benki ya TPB,  Deogratius Kwiyuka akimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sabasaba Moshigi na kuhudhuriwa pia na Uongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU) ambao ndiyo wamiliki wa shule hiyo.


Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya makabidhiano hayo,Mkurugenzi wa Masoko wa Benki hiyo Kwiyuka, amesema wanaunga Juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuboresha elimu hapa nchini, hivyo wao kama wadau wakubwa wa elimu wakaona ni vyema kutoa msaada huo wa rangi ili kuboresha mandhari nzuri ya shule hiyo ya sekondari Buluba.

Amesema shule inapokuwa katika mandhari nzuri inaleta ari ya wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo yao na kupata ufaulu mkubwa, huku akitoa wito kwa wanafunzi wa shule hiyo ya Sekondari Buluba kujituma kwenye masomo ili waje kuwa tegemezi katika familia zao na taifa kwa ujumla.

“Benki ya TPB huwa tunahusika na masuala ya Ustawi wa Jamii, Afya pamoja na Elimu, hivyo kutokana na sisi kuwa wadau wakubwa wa elimu tumetoa sehemu ya faida ya beki ili kutoa msaada huu wa rangi kwa ajili ya kupendezesha shule ya Sekondari Buluba na kuiweka katika mandhari nzuri,”amesema Kwiyuka.

Naye Mwalimu wa Shule hiyo, Emmanuel Kazyoba akisoma risala ya shule hiyo, amesema ina miaka 50 ambapo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu na kupongeza msaada huo wa rangi ambao utasaidia kuipendezesha shule hiyo.

Amesema licha ya kukabiliwa na uchakavu wamekuwa wakifanya vizuri kwenye masomo ambapo matokeo ya kidato cha sita mwaka huu (2019), daraja wa kwanza wamefaulisha wanafunzi 4, daraja la pili 24, la tatu 46, la nne 10 pamoja na zero moja,

Kwa upande Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) Richard Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo, amepongeza msaada huo wa rangi na kuahidi kuendelea kusimamia ufaulu wa shule ambapo wametoka kwenye zero saba mwaka jana hadi moja.


Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi wa Masoko kutoka Benki ya TPB Makao makuu Deogratius Kwiyuka, akizungumza wakati wa kukabidhi ndoo za rangi 50 kwenye shule ya sekondari Buluba Shinyanga Mjini kwa ajili ya kupendezesha shule hiyo na kuwa katika mazingira mazuri na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Meneja wa Benki ya TPB tawi la Shinyanga, Faraji Basso, akizungumza kwenye kukabidhi ndoo za rangi 50 katika shule hiyo ya sekondari Buluba.


Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), Richard Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi wa shule ya sekondari Buluba, akishukuru kwa msaada huo wa ndoo za rangi, na kuahidi kuendelea kuboresha miundombinu ya shule hiyo.


Ndoo za rangi 50 zikiandaliwa kwa ajili ya kukabidhiwa kwenye shule ya Sekondari Buluba.

Mkurugenzi masoko kutoka Benki ya TPB Makao makuu Deogratius Kwiyuka (kulia) akikabidhi ndoo za rangi 50 kwa ajili ya kupendezesha shule ya Sekondari Buluba, katikati ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) Richardi Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo na Meneja wa (SHIRECU) Ramadhani Kato wakipokea rangi hizo.

Mkurugenzi wa masoko kutoka benki ya TPB Deogratius Kwiyuka katikati akikabidhi ndoo za rangi 50 katika shule ya Sekondari Buluba kama sehemu ya faida kwenye benk hiyo, wa kwanza kulia ni mwanafunzi Thomas Majuto,na mwisho kushoto ni meneja wa (SHIRECU) Ramadhani Kato, akifuatiwa na mwenyekiti wa SHIRECU Richard Luhende.

Mkurugenzi wa masoko kutoka benk ya TPB makao makuu Deogratius Kwiyuka, akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi rangi ndoo 50 katika shule ya sekondari Buluba.

Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU) Mkoani Shinyanga Ramadhani Kato akishukuru kwa kupokea msaada huo wa ndoo za rangi zilizotolewa na benki ya TPB kwa ajili ya kuweka mandhari nzuri ya shule hiyo.

Awali Mwalimu wa shule ya Sekondari Buluba Emmanuel Kazyoba, akisoma taarifa ya shule hiyo na kuelezea kuwepo na changamoto ya uchakavu wa majengo ambapo rangi hizo zitasaidia kuiweka shule katika mandhari nzuri.

Mwanafunzi Thomas Majuto akishukuru kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya sekondari Buluba kuhusu msaada huo wa rangi na kuahidi kujituma kusoma kwa bidii ilikuongeza ufaulu katika shule hiyo.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Buluba wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa rangi ndoo 50 kutoka benki ya TPB.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Buluba wakisikiliza nasaha za kusoma kwa bidii ili waje wasaidie familia pamoja na taifa kwa ujumla.

Wafanyakazi wa (SHIRECU) wakiwa kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa rangi ndoo 50 kutoka Benki ya TPB.
Picha zote na  Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527