AMCHINJA BABA YAKE AKIDHANI NI MBUZI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, July 18, 2019

AMCHINJA BABA YAKE AKIDHANI NI MBUZI

  Malunde       Thursday, July 18, 2019

Mwanaume mwenye umri wa miaka 29 anadaiwa kumuua baba yake kwa kumkata shingo akifikiri alikuwa anachinja mbuzi.


Tukio hilo lilitokea siku ya Jumanne Julai 17, katika eneo la Nanyuki, Kaunti ya Laikipia, Kenya.

Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Dennis Mwangi anadaiwa kumchinja baba yake mzazi Peter Ndegwa mwenye umri wa miaka 59.

Kwa mujibu wa gazeti la Taifa Letu la Kenya, inadaiwa mtuhumiwa huyo alimkata shingo na kutenganisha kichwa na kiwiliwili cha baba yake aliyekuwa akiugua kwa muda mrefu.

“Baada ya kufanya unyama huo, mtuhumiwa alikiweka kichwa hicho katika ndoo na kuzunguka nacho mjini Nanyuki,” alisema shuhuda ambaye hata hivyo, hakutaka kutaja jina lake.

Jeshi la Polisi limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba linamshikilia mtuhumiwa huyo kwa uchunguzi zaidi.

Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Laikipia Mashariki, Kizito Mtoro alisema baada ya mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kumuua baba yake na kusema kuwa alidhani alikuwa akimchinja mbuzi.

“Maafisa wa polisi hawakuweza kubainisha nia ya mauaji hayo mara moja. Uchunguzi unaendelea na taratibu zikakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili kufunguliwa mashtaka yanayomkabili.”

Mwangi ambaye alikuwa mfanyabiashara maarufu na mmliki wa duka kubwa mjini Nakuru pia aliwahi kuwania kiti cha useneta katika uchaguzi mkuu uliopita 2017.

Mmoja wa wakazi wa Nanyuki, Enny Shii alisema “kumekuwa na visa vingi vya kutatanisha. Tunahitaji maombi,”

Mwezi uliopita, mwanamme mmoja aliripotiwa kumuua mama yake mzazi katika Kijiji cha Matanya karibu na mpaka wa Kabanga na Kamangura huku mwanamme mmoja akiripotiwa kumuua mpenzi wake ambaye pia alikuwa mke wa mtu.

Taifa Leo Dijitali inaomba radhi kwa wasomaji kuhusu maelezo ya kutisha na kuogofya ya jinsi mshukiwa ameripotiwa kutekeleza mauaji hayo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post