WAHUNI WAVUNJA KANISA NA KUIBA SADAKA

Polisi kaunti ya Baringo nchini Kenya wanalisaka kundi la wezi ambao wamevunja kanisa la Full Gospel Kabarnet na kutoweka na mali pamoja na pesa taslimu 'sadaka'. 

Wizi huo ulifanyika Jumamosi usiku, Julai 13,2019 huku washirika wakiamkia mshangao siku ya Jumapili na hali hiyo kutatiza ibada.

Duru zimearifu  kuwa wezi hao walivunja eneo ambalo sadaka ilikuwa imefichwa baada ya kuingia kanisani na kutoweka na fedha hizo.
 "Tumeamka asubuhi na kupata waliiba kila kitu. Tunashuku ni vijana tu wa mtaa huu," mmoja wa viongozi wa kanisa hilo alisema. 

Washirika wa kanisa hiyo walisema hilo ndilo tukio la wizi la kwanza kwenye kanisa hiyo katika kipindi cha miaka 40.
Chanzo - TUKO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527