MWALIMU AJIKATA SHINGO KWA CHUPA ILI AFE AKIDAI MAISHA MAGUMU


Mwalimu wa Shule ya Msingi Rung’abure iliyopo Serengeti Mkoani Mara, Godfrey Tarimo amejikata na chupa eneo lake la shingo katika jaribio la kutaka kujiua kwa kile alichosema ni kuzidiwa na ugumu wa maisha na mahusiano mabaya na jirani zake.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nyerere, Wilaya ya Serengeti, Dkt Tanu Warioba amethibitisha kumpokea mwalimu usiku wa Julai 3, 2019 akiwa ameletwa kwa msaada wa walimu wenzake.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema hatua kali za kinidhamu na sheria zitachukuliwa kwa mwalimu huyo ikiwezakana hata kufukuzwa kazi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527