WAREMBO 13 KESHO KUCHUANA FAINALI SHINDANO LA MISS SHINYANGA 2019



Jumla ya warembo/walimbwende 13 kutoka halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kishapu,Kahama Mji, Ushetu,Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga kesho watachuana kuwania taji la Miss Shinyanga 2019.


Fainali ya Mashindano ya kutafuta Mrembo wa Mkoa wa Shinyanga(Miss Shinyanga 2019) yatafanyika kesho Jumamosi kuanzia saa moja kamili katika ukumbi wa CCM Mkoa (NSSF ya Zamani Mjini Shinyanga).

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Burudani ya Makumbusho Entertainment ambao waandaaji wa Shindano la Miss Shinyanga 2019, George Foda amesema maandalizi yamekamilika hivyo kuwaomba wakazi wa Shinyanga na maeneo ya jirani kufika kujionea jinsi wanavyoonesha vipaji vyao katika tasnia ya urembo ya ubunifu.

Amesema zawadi ya pesa taslimu na ufadhili wa masomo ya vyuo mbalimbali kwa washiriki wa mashindano hayo zitatolewa.

Miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza katika mashindano hayo ni Linah Sanga,Daz Baba na Five Star Modern Taarabu.
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Washiriki wa Shindano la Miss Shinyanga 2019.

Washiriki wa Shindano la Miss Shinyanga 2019.


Washiriki wa Shindano la Miss Shinyanga 2019.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527