MTOTO WA MAKONDA KATIMIZA MWAKA MMOJA.....TAZAMA UJUMBE ALIOUNDIKA KWA AKINA WANAOHANGAIKA KUPATA WATOTO


Kupitia ukurasa wa instagram, Paul Makonda ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam  ameandika ujumbe kwa kina mama wanaohangaika kupata mtoto, walioteseka na kudharaulika na hadi wengine kufikia hatua ya kuitwa mpaka tasa 

==>>Kupitia ujumbe huo amewaomba wanawake hao wasikate tamaa. Usome hapo chini


Ninapokumbuka siku kama ya leo Kwa mwaka uliopita nayaona machozi Mengi ya furaha kwangu kwa mke wangu na ndg zangu juu ya Muujiza huu Mkubwa ktk maisha yetu.

Kwa sababu hii naomba niseme jambo moja kwa Wakina mama wengi sana ambao wamebakia na vidonda vya kudumu moyoni baada ya morning kuchukiwa,kusingiziwa vya uongo na kutuhumiwa na ndugu au waume zao kwa kukosa watoto.Wengi tunasahau kuwa mtoto ni zawadi anayotupa Mungu.

Wapo ambao hadi wameachwa huku wakinenewa maneno magumu ya kuvunja moyo.Leo ningependa niwape pole wote mliopitia nyakati hizi katika maisha yenu.

Jambo kubwa ambalo ningependa kukumbusha ni kuwa pamoja na juhudi za kibinadamu za kidaktari,pamoja na maombi ya kila aina tunayoweza kufanya mbele za Mungu,pamoja na mipango mingi kuhusu kupata mtoto:JIBU LA MWISHO HUTOKA KWA MUNGU.

Mama yangu unayepitia changamoto hii endelea kumtumaini Mungu ATAFANYA KWA WAKATI WAKE kwani yeye HAWAHI wala HACHELEWI.

Nakuombea kwa Mungu,Usife Moyo.Ipo siku utaitwa mama ewe ulieitwa Tasa Kwa jina la Yesu mwana wa Mungu aliye hai.

Amen
Ni Mimi Paul Makonda ndg yako katika Kristo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post