MISRI YATUPWA NJE AFCON KWA KUCHAPWA BAO 1-0 NA AFRIKA KUSINI

Mabingwa watetezi Cameroon na wenyeji Misri wameyaaga mashindano Jumamosi Juni 6 baada ya kutolewa kwenye siku ya pili ya hatua ya mtoano.


Cameroon na Misri ndio waliocheza fainali ya Kombe la Maifa ya Afrika (Afcon) miaka miwili iliyopita ambapo Cameroon ilitwaa ubingwa.

Hata hivyo timu hizo mbili zimeyaaga mashindano baada ya Cameroon kufungwa 3-2 dhidi ya Nigeria jijini Alexandria.

Misri wamepigwa mbele ya mashabiki elfu sabini jijini Cairo na Afrika Kusini kwa goli moja tu lililofungwa na Thembinkosi Lorch katika dakika ya 85.

Afrika Kusini ambao walifuzu katika raundi ya mtoano kama timu ya tatu kwenye kundi lao baada ya kushinda mchezo mmoja tu haikupigiwa upatu katika mechi ya hiyo dhidi ya Misri inayoongozwa na mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah.

Umakini wa safu ya ulinzi wa Afrika Kusini  ndio imekuwa chachu ya ushindi baada ya kuhimili vishindo na mikiki ya safu ya ushambuliaji ya Misri ambayo iliibuka na ushindi kwenye mechi zote tatu za makundi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527