MAKAHABA WAMLILIA RAIS AWASAIDIE...WADAI SASA BIASHARA NGUMU

Kundi la makahaba kutoka eneo la Gilgil Kaunti ya Nakuru nchini Kenya limejitokeza na kuomba usaidizi kutoka kwa serikali. Wakiongea Jumanne, Julai 2, 2019 makahaba hao walisema kazi yao imekuwa ngumu sana na wanataka serikali kuingilia kati na kuwasaidia ili wajikimu kimaisha. 

Wakati uo huo, walimuomba Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kusikiliza kilio chao kwani wako tayari kuiacha kazi hiyo iwapo watapata msaada wa serikali ili kuanza kazi nyingine.

"Tunaililia serikali, Rais Uhuru pamoja na mdogo wake aki tusaidieni ... kama vile huwa tunaona mkisaidia wazee na walevi pia tunaomba usaidizi. Na tuko tayari kuiacha kazi hii," mmoja wao alisema.

 Wafanyabiashara hao wa masuala ya ufuska walikuwa wakizungumza wakati wa mahojiano na gazeti la Nation.

 Vile vile wanaitaka jamii kukoma kuwaona kama watu waliopotoka kimaadili huku wakisema ni shida zimewasukuma kushiriki biashara hiyo.

 "Hakuna haja ya kutukejeli eti huyo huyo sex worker ... si kupenda kwetu kujiuza kimwili, na si rahisi. Unaweza ukakufa uwache bibi yako na ajiuze kimwili na si kwa kupenda," alisema mmoja wao. 

Ukahaba nchini Kenya ni kinyume cha sheria.

 Hata hivyo, mamia ya vipusa wamejitosa katika miji mikuu kujizolea riziki wakitumia mili yao.

 Jijini Nairobi, barabara ya Koinange ni maarufu kwa biashara ya ngono na wakati mmoja mwaka wa 2003 wabunge walikamatwa eneo hilo usiku wa manane wakiwanyemelea vipusa waliokuwa nusu uchi. 

Mjini Nakuru, eneo la Kikopey, Gilgil, barabara ya Gusii na pia eneo la kibiashara la Salgaa ni baadhi ya ngome kuu ambapo wasichana hunadi mili yao peupe. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527