MO DEWJI AJIBU KUHUSU KUJIONDOA SIMBA.......'KAA MBALI SANA NA WATU WENYE NIA MBAYA'


Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba ambaye ni mwekezaji wa timu hiyo, Mohammed Dewji, amejibu taarifa kuhusu kujiondoa Simba.

Taarifa hizo zilianza kusambaa usiku wa jana katika mitandao ya kijamii, lakini mwenyewe amejitokeza na kuweka bayana kinachoendelea.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mo Dewji amesema, "watu wenye nia mbaya. Kazi yao sio kujenga, ni kuvunja tu. Kaa nao mbali. Narudia kaa nao mbali sana!".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527