BABU MATATANI KWA TUHUMA YA KUBAKA NA KULAWITI WATOTO WATANO WA DARASA LA TATU



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Hamisi Issah

Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro, linamshikilia mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Yahya Idd, Mkazi wa Njoro kwa tuhuma za kubaka na kulawiti watoto 5, wanaosoma darasa la tatu katika shule ya Msingi Chemchem, iliyopo Manispaa ya Moshi.

Akizungumza leo Julai 16, kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamis Issah amesema, tukio hilo limetokea Julai 15, baada ya watoto hao wenye umri kati ya miaka nane na kumi, kufanyiwa ukatili huo wakati wa mapumziko.

Kwa mujibu wa kamanda imeelezwa kuwa, watoto hao walitoroka shuleni na baada ya kurejea, mmoja wa wale watoto alikuwa anatembea huku akichechemea na baada ya kuhojiwa walidai wametoka kwa babu Yahya.

Na kwamba uchunguzi wa awali, umeonyesha watoto hao kubakwa, huku mmoja akiwa amelawatiwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527