ASKARI 8 WALIOTUHUMIWA KUTOROSHA MADINI JIJINI MWANZA WAACHIWA HURU


Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imewaachia huru Askari nane waliokuwa wakikabiliwa na kesi namba 01 ya 2019 ya uhujumu uchumi kwa kutorosha madini ya dhahabu.


Maamuzi hayo yametolewa na Hakimu Mkazi Rhoda Ngimilanga katika Mahakama ya Mkoa wa Mwanza baada ya kusikiliza pendekezo la upande wa mashtaka uliotaka shauri hilo liondolewe Mahakamani na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kwa kuonesha nia ya kutotaka kuendelea na shauri hilo.

Hakimu Rhoda amesema Mahakama imewaondolea mashtaka watuhumiwa hao na wapo huru baada ya DPP kuwasilisha ombi hilo.


Uamuzi huo wa Mahakama umefanywa baada ya jana Jumatano, DPP, Biswalo Mganga kutangaza kuifuta kesi namba moja ya mwaka 2019 ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili askari hao.

Biswalo alisema kesi hiyo imefutwa kwa sababu ya maslahi ya Taifa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527