ZAIDI YA NG’OMBE, 20000 USHETU HATARINI KUKUMBWA NA UGONJWA UNAODHANIWA KUWA NI WA MIGUU NA MIDOMO

SALVATORY NTANDU

Zaidi ya mifugo 20,000 aina ya Ng’ombe  katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga iko hatarini kukumbwa na ungonjwa unaodhaniwa kuwa ni wa miguu na midomo ulioibuka katika kata tatu na kusababisha vifo vingi vya mifungo.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana mwenyekiti wa Chama cha wafugaji wilayani Kahama (CCWT), DOA LIMBU ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyankende katika Halmashauri hiyo amesema ugonjwa huo umeripotiwa katika kata za Chambo,Chona na Nyakende.

Amesema ugonjwa huo unathiri mifugo hasa sehemu za maini na mapafu na kuiomba serikali kuchukua hatua za haraka kwa kutoa elimu kwa wafugaji ili waweze kutambua kwa haraka dalili za ugonjwa huo pindi unapobainika.

DOA amefafanua kuwa mwaka jana serikali ili toa chanjo wa mifugo yote katika Halmashauri hiyo na wao walisimamia kikamilifu zoezi hilo ambalo lilifanikiwa kwa kiwango kikubwa lakini kuibuka kwa ugonjwa huo huenda ikachangiwa na mwingiliano wa mifugo kutoka mikoa ya jirani ya Geeita, kigoma na Tabora.

Mbali na hilo DOA amewataka wafugaji wote kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa mifugo wanaotembelea maeneo yao ili kuhakikisha ugonjwa huo unapatiwa tiba pamoja na kutokula vitoweo vya mifugo iliyobainika kuwa na ugonjwa  huo.

Katika Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya habari na Mkuu wa wilaya ya Kahama June 11, ANAMRINGI MACHA amesema tayari wataalamu wa  mifugo kutoka ofisi ya kanda ya mwanza wamekwisha fika katika maeneo hayo na kuchukua sampuli kwaajili ya vipomo ili kuchukua hatua zaidi.

MACHA amesema katika hatua za awali za kudhibiti ugonjwa huo  ni vyema wafugaji wa maeneo yaliotajwa wasitoe mifugo nje wala kuingiza katika maeneo yaliyoathirika wakati serikali ikichukua hatua za haraka ili kuutokomeza ugonjwa huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post