BIASHARA MPYA KUSAMEHEWA KODI KWA MIEZI 6 YA MWANZO

Serikali  imependekeza kusamehe kodi mfanyabiashara au mwekezaji kwa kipindi cha miezi sita pindi anapopewa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).


Msamaha huo, utaanza kutumika Julai Mosi 2019, ili kumuwezesha mfanyabiashara au mwekezaji kujiandaa na mahitaji yanayotakiwa katika shughuli anazofanya.

Vile vile kuondoa usumbufu, dhana ya woga wakati wa kuanza biashara ikiwamo mahitaji ya leseni ya biashara na vibali vingine.

Hayo yameelezwa jana  Alhamisi Juni 13, 2019 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phili Mpango wakati akiwasilisha makadirio na mapato ya Serikali kwa mwaka 2019/20.

Waziri Mpango alisema, “Hatua hii inatofautiana na hali ilivyo sasa ambapo mfanyabiashara anapopewa TIN anaanza kufanyiwa tathimi (tax assessment) ya mapato yake ya biashara na kutakiwa kulipa kodi.”


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post