MWANAFUNZI ALIYEPIGWA RISASI AKIINGIA IKULU AGOMA KULA

Brian Kibet Bera, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha JKUAT  nchini Kenya aliyepigwa risasi akijaribu kuingia Ikulu amedaiwa kugoma kula.

Bera anaendelea kupata nafuu siku kadhaa baada ya kisa chake kugonga vichwa vya habari ndani na nje ya Kenya na baadaye kulazwa katika Hospitali Kuu ya Kitaifa ya Kenyatta. 

 Ripoti zilizozuka Alhamisi, Juni 13 zilisema, mwanafunzi huyo alisusia kwa muda chakula kwasababu zisizojulikana. 

Baba yake mzazi David Bera amekuwa hatulii na akihojiwa na wanahabari alisema mwanawe hana akili timamu.

“Kwa sababu ambazo siwezi kusema hajala leo, sio kama jana,” David Bera aliiambia K24. 

Brian anaendelea kupata nafuu chini ya ulinzi mkali na anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiakili katika Hospitali ya Mathari mara akionyesha dalili za kupona jeraha za risasi aliyopigwa. 

Hata hivyo, ikiwa ataendelea kususia chakula, basi huenda atakaa sana hospitalini kinyume na ilivyotarajiwa. 

Siku mbili baada ya kisa chake, Brian hangeweza kukumbuka kilichotokea na hali hiyo ikaelekea kubaini kuwa hana akili timamu.

 Pia baba yake amefichulia vyombo vya habari kuwa, mwanawe amefanya mambo mengine ya kutisha awali na wakati mmoja Brian alijaribu kukweya Mlima Kenya. 

Chanzo - Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post