Breaking News : WEMA SEPETU ATUPWA MAHABUSU SIKU SABA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, June 17, 2019

Breaking News : WEMA SEPETU ATUPWA MAHABUSU SIKU SABA

  Malunde       Monday, June 17, 2019

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemuamuru Msanii Wema Sepetu kwenda gerezani siku saba mpaka Juni 24 akisubiria uamuzi wa mahakama wa kumfutia dhamana. 

Nyota huyo wa filamu anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono mitandaoni kupitia simu yake ya kiganjani.


Uamuzi huo wa Mahakama umefikiwa leo Juni 17, mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde wakati mshtakiwa huyo alipofikishwa mbele yake.


Wakili wa Serikali Glory Mwenda amedai mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa hapo baada ya mahakama wiki iliyopita kutoa hati ya kumkamata Wema kwa kosa la kuruka dhamana.


Hakimu Kasonde alimtaka Wema kujieleza kwanini asifutiwe dhamana kwa kushindwa kufika mahakamani kwa tarehe mbili tofauti.


Akijieleza Wema alidai Mei 14 mwaka huu hakufika sababu alikuwa safarini mkoani Morogoro na Juni 11 mwaka huu aliumwa akashindwa kupandisha mahakamani.


Mshtakiwa aliomba msamaha na Wakili wa Serikali, Mwenda aliomba Mahakama impe onyo mshtakiwa ili asirudie kufanya kitendo hicho chenye usumbufu.


Hakimu Maira alisema kasikia hoja zilizowasilishwa na atapitia kiapo cha mshtakiwa kisha atatoa uamuzi Juni 24 mwaka huu na akaamuru katika kipindi cha kusubiri uamuzi mshtakiwa akae rumande.


Wema anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa hazina maudhui.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post