TRUMP KASEMA KILICHOMFANYA ASIISHAMBULIE KIJESHI IRANI NI KUHOFIA VIFO VYA WATU 150.....JANA IRAN ILIITUNGUA NDEGE MOJA YA MAREKANI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 21, 2019

TRUMP KASEMA KILICHOMFANYA ASIISHAMBULIE KIJESHI IRANI NI KUHOFIA VIFO VYA WATU 150.....JANA IRAN ILIITUNGUA NDEGE MOJA YA MAREKANI

  Malunde       Friday, June 21, 2019

Rais wa Marekani Donald Trump amesema leo kuwa alisitisha shambulizi la kijeshi dhidi ya Iran kwa sababu jibu kama hilo kwa hatua ya Iran kutungua ndege ya Marekani isiyoruka na rubani lingesababisha idadi kubwa kabisa ya vifo. 

Katika mfululizo wa ujumbe aliondika kwenye mtandao wa Twitter, Trump amesema vikwazo vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Iran vinafanya kazi na vingine vimetangazwa jana usiku kufuatia kuharibiwa kwa ndege ya Marekani isiyoruka na rubani iliyotunguliwa na kombora la Iran.

Trump amesema mpango ulikuwa ni kulipua maeneo matatu tofauti ya Iran kama jibu la kitendo cha Iran, na kuwa aliambiwa watu 150 wangeuawa na ndio maana akasitisha shambulzii hilo zikiwa zimesalia dakika 10 tu kwa ndege za Marekani kufyatua makombora.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post