BIASHARA UNITED KUSAJILI WACHEZAJI WAPYA 13


Katibu wa Biashara United Haji Mtete
Na Asha Shaban - Mara.

Timu ya soka ya Biashara United Mara inatarajia kusajili wachezaji wapya 13 ikiwa ni mikakati ya kukisuka kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya michuano ijayo ikiwemo ligi kuu msimu ujao.

Aidha timu hiyo pia inatajia kuwaacha wachezaji wake 12 kutokana na viwangio vyao kutorodhisha kwa muda waliokuwa na timu hiyo katika msimu wa ligi kuu uliopita

Katibu wa Biashara United Haji Mtete alisema kutokana na wachezaji hao kushidwa kuwa na viwango bora katika msimu ulio pita ndio sababu ya kuachwa katika msimu unao kuja wa michuano hiyo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Alisema mbali na kuachwa kwa wachezaji hao 12 wanategemea kusajili wachezji wengine 13 ambao wataungana na wale walio bakia na kuunda kikosi kilicho bora ambacho kitakuwa ni cha ushindani katika msimu ujao

Mtete alisema tayari wameisha kaa kikao cha kamati tendaji nakujadiliana namna ya kuwapata wachezaji wengine hao 13 ambao watatakuwa na timu msimu ujao ambapo alisema tayari kamati ya usajili imeisha undwa tayari na itakuwa inapitia wachezaji mbalimbali na kusajiliwa.

Alisema biashara united imejipanga kikamilifu katika msimu wa usajili wa ligi kuu ijayo ya msimu wa mwaka 2019/20 kwa kuhakikisha inafanya vizuri katika michuano hiyo ya ligi kwa kuwa na wachezaji wenye ari ya kimichezo muda wote.

Aliongeza kuwa timu ya biashara pia itafanya kikao na wadau watimu hiyo siku ya tarehe 23 ya mwezi juni lengo likiwa ni kuzungumza na wadau na mashabiki wa timu hiyo kwa kupokea mapendekezo yatakayo tolewa kutoka kwa wanachama na wapenzi wa timu hiyo

Alisema kama ilivyokuwa msimu uliopita kuwa biashara ilikuwa ni timu ya wananchi wa mkoa wa mara bado anaendelea kuwaomba wana mara kuendelea kuichangia timu yao kama ambavyo walikuwa wanafanya msimu uliopita na kuwezesha timu hiyo kubakia katika ligi kuu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527