SERIKALI YAAHIDI KUUPIGA JEKI MCHEZO WA WAVU MKOANI MWANZA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, June 13, 2019

SERIKALI YAAHIDI KUUPIGA JEKI MCHEZO WA WAVU MKOANI MWANZA

  Malunde       Thursday, June 13, 2019

Serikali imeahidi kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili mchezo wa wavu ambao ni miongoni mwa  michezo iliyosahaulika licha ya kuwa ni mchezo wenye kuvutia watu wengi na unaweza kutumika kama sehemu ya watu kujiajiri.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati alipokuwa akifungua mashindano ya wavu ya Afrika Mashariki katika viwanja vya Milongo   yajulikakanayo kwa jina la Jembe Mirjan East Africa Volleyball Championship yanayofanyika jijini Mwanza.

Mashindano hayo yana shirikisha timu sita  na yatafanyika ndani ya muda nne ambapo mashindano hayo yameanza kati ya timu ya MTC Nyegezi dhidi ya Polisi Zanzibar ambapo mchezo  umemalizika huku Zanzibar Polisi wakiongoza kwa goli 39 kwa 30

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo, Mhe.Kanyasu amewataka wachezaji wawe wavumilivu kutokana na changamoto wanazozipitia kwa vile mchezo wa wavu mbali na mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo ambao umekuwa ukikosa Wadhamini kwa sababu haujaweza kufahamika kiasi cha kuwashawishi Wadhamini kuweza kuweka pesa zao.

Amewaeleza wachezaji hao kuwa  lazima wakubali kuumia  kwanza kwa hiki kipindi cha mwanzo ili baadaye wadhamini waweze kujitokeza.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewahakikishia waandalizi wa mchezo huo kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro itadhamini mchezo huo kama ilivyokuwa imeahidi mwanzo

Naye,  Meneja wa Jembe FM, Fredy Kikoti amesema mchezo huo umekuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi ikiwa pamoja na kukosekana kwa wadhamini hali iliyopelekea baadhi ya timu kushindwa kushiriki katika mashindano hayo.

Amesema mashindano hayo tangu yalipoanzishwa mwaka jana yamekuwa chanzo cha  kuibua vipaji kwa vijana wa Kanda ya ziwa pamoja na Tanzania kwa
 Ujumla

Mashindano hayo ya Afrika Mashariki yameanza Juni 12 mwaka huu yanatarajia kumalizika Juni 16 mwaka huu katika viwanja vya Milongo

Mwisho


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post