WABUNIFU WALIOBUNI MTAMBO MDOGO WA KUFUA UMEME WAPEWA MAMILIONI YA MTAJI


Rais John Magufuli ameliijia juu Shirika la umeme nchini (Tanesco) kwa kushindwa kuwaunga mkono wabunifu waliobuni mtambo mdogo wa kufua umeme kwa kutumia maji ya mto Mkoani Njombe, na kuwataka kuwalipa wabaunifu hao fedha watakazozitumia kama kianzio cha kununua vifaa kwaajili ya shughuli zao.


Ametoa tamko hilo leo Alhamisi Juni 13, Ikulu jijini dare s salaam alipokua akizungumza na wananchi hao John Mwafute maarufu Mzee Pwagu na Ngairo ambapo ameamuru shirika hilo kuondoka na wabunifu hao haraka iwezekanavyo na kwenda kukagua mradi huo ili kujua namna unavyofanya kazi.

“Tanesco hakikisheni mnaondoka na hawa waliozalisha umeme kwenda kuangalia hiyo mitambo na kuweka kinga maana mlitakiwa muwape ushirikiano kuanzia mwanzo lakini hamkufanya hivyo, na wasiondoke na basi kama walivyokuja mchukue magari yenu yenye nembo ya Tanesco,” amesema.

“Tanesco ndio mlitakiwa kuwasaidia hawa lakini muwakilishi wenu mliyemuweka anasema mpaka watakapokuja akiwa amekaa kwenye kiti anazunguka huku amevaa miwani meusi wakati yuko ofisini na jua halimchomi wakati angekuwa ameshaenda pale na kuuona huo mradi,” amesema.

Aidha amewataka viongozi kuwa na utaratibu wa kuangalia runinga ya taifa na kufuatilia kitu chochote kitakachokuwa kinatolewa kinachohusu wizara zao ili waweze kuvifanya kazi.

Wabunifu hao wamekabidhiwa shilingi milioni 7.5 kila mmoja kutoka kwa rais Magufuli huku Tanesco wakiahidi kutoa shilingi milioni 15 kwa kila mmoja, nayo Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) imeahidi kutoa shilingi milioni 10 kwa kila mmoja kama kianzio cha kuwasaidia wabunifu hao kujiendeleza.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post