MWIGULU NCHEMBA ATAKA STAILI YAKE YA KUVAA SKAFU SHINGONI ITAMBULIWE KAMA VAZI RASMI LA TAIFA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, June 17, 2019

MWIGULU NCHEMBA ATAKA STAILI YAKE YA KUVAA SKAFU SHINGONI ITAMBULIWE KAMA VAZI RASMI LA TAIFA

  Malunde       Monday, June 17, 2019

Mbunge wa Iramba Magharibi Dr. Mwigulu Nchemba amependekeza kuwa mtindo wa mavazi ambao yeye amekuwa akiuvaa mara kwa mara utumike kama vazi la taifa kwa kile alichokieleza umekuwa ukiwatambulisha watanzania hasa wanapokuwa nje ya nchi.


Dr. Mwigulu ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akiuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo juu ya vazi rasmi la taifa.

Mwigului Nchemba ameuliza kuwa "watanzania wakienda nje ya nchi wanatumia skafu, tai bendera ya taifa yani Mwigulu style na wanatambuliwa ni Watanzania, kwanini Serikali isiseme hili ndilo vazi la taifa?.

Akijibu swali hiyo, Naibu Waziri Juliana Shonza amesema kwa sasa mchakato wa kulipata vazi la taifa ulishaanza upya hivyo watahakikisha wanapokea maoni ya watu mbalimbali.

"Kwa sababu mchakato umeshaanza, nimwambie tu maoni ambayo ameyatoa tunayachukua na tutayafanyia kazi", amesema shonza.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post