MAREKANI YAKASIRISHWA NA VITISHO VYA IRAN


Marekani haijafurahishwa na vitisho vilivyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif katika mkutano na mwenzake wa Ujerumani Heiko Maas mjini Tehran. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni ya Marekani amesema kuwa Iran inachagua moja rahisi tu, ijionyeshe kuwa nchi ya kawaida au ishuhudie uchumi wake ukisambaratika. 

Zarif aliituhumu Marekani kwa kufanya vita vya kiuchumi kutokana na vikwazo ilivyoiwekea Iran na akaonya kuwa wale wanaounga mkono vita wasitarajie kuwa salama. 

Maas anataka kuyaokoa makubaliano ya nyuklia na Iran, lakini hakupiga hatua zozote za maana wakati wa ziara yake nchini humo. 

Maas alisema jana kuwa Ujerumani itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa mvutano hauongezeki kati ya Marekani na Iran.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527