IRAN YAZINDUA MFUMO WA MAKOMBORA WA KHORDAD 15

Iran imezindua mfumo wa kujilinda kwa makombora unaoweza kulenga shabaha sita za adui kwa wakati mmoja.


Mfumo huo wa makombora uliopewa jina la Khordad 15 umezinduliwa mbele ya Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Amir Hatami. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Brigedia Jenerali Hatami amesema kuwa, mfumo wa makombora wa Khordad 15 una uwezo wa kugundua ndege za kivita na droni kutoka umbali wa kilomita 150 na kuzifuatilia katika umbali wa kilomita 120.

Ameongeza kuwa mfumo huo wa makombora aidha una uwezo wa kugundua maeneo ya siri na kuyasambaratisha katika umbali wa kilomita 45.

Waziri wa Ulinzi wa Iran ameeleza pia kwamba mfumo wa ulinzi wa Khordad 15 unatumia makombora ya Sayyad 3; na una uwezo wa kugundua, kusambaratisha na kutungua shabaha sita kwa wakati mmoja.

Iran imeeleza kuwa uwezo wake wa kijeshi ni kwa ajili ya kujilinda na si tishio kwa nchi nyingine.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527