JAMAA AJIGAMBA KULALA NA WANAWAKE ZAIDI YA 1000...ADAI 'WANAWAKE HAWAANGALII SURA '

Tafadzwa ni mchimbaji wa madini anajivunia tabia yake ya kuwatumia wanawake atakavyo

Mmoja wa makaka mapacha wenye utata nchini Zimbabwe wanaofahamika kama Fichani twins, ambao waliwahi kugonga vichwa vya habari kwa kukukusanya umati wa watu katika mitaa ya mji mkuu wa Zimbabwe Harare mwaka 2006 walipovaa vipande vya ngozi ya mbuzi zilizoficha tu sehemu zao za siri amedai kuwa amekwishalala na wanawake zaidi ya 1000.

Gazeti la New Zimbabwe limeripoti kuwa Tafadzwa Fichani ambaye kwa sasa anaishi katika eneo la kati nchini humo la Gokwe Nembudzi ameliambia kuwa kwa sasa anaishi na virusi vya HIV na sasa ni mgonjwa wa Ukimwi na hivyo hajali kwa kiasi kwamba hatumii kinga yoyote ya kuzuia maambukizi hayo.

"Ni kwanini nitumie mipira ya kondomu wakati sasa ninafahamu kuwa nimeathirika na HIV, nijilinde ili iweje sasa?" Tafadzwa aliuliza huku akijigamba.

Tafadzwa ni mchimbaji wa madini , akiendesha biashara zake katika eneo lenye shughuli za uchimbaji madini la Zenda na anajivunia tabia yake ya kuwatumia wanawake atakavyo.Maeneo ya uchimbaji wa Madini nchini Zimbabwe yana idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya HIV

" Nimelala na zaidi ya wanawake 1000. Kile ninachoweza kukwambia ni kwamba wanawake hawajali muonekano wa sura, kile wanachoitaka ni pesa ," Tafadzwa aliliambia gazeti la NewZimbabwe.com na kuongeza kuwa amekuwa muathiriwa wa utajiri wake.

"Pesa zangu zote nilizopata kutokana na madini, nimezitumia kuwafurahisha wanawake na hicho ndicho wanawake wanachokitaka. Pesa hapa sio tatizo.''

Shirika la taifa la kupambana ma Ukimwi nchini Zimbabwe limeripoti kuwa eneo la Gokwe Nembudziya pekee lina viwango vya maambulkizi ya HIV kati ya 8-10% na wachimba wa madini ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa cha maambukizi hayo.

Kwa mujibu wa Tafadzwa mwanamke anayemfuata mchimbaji madini huwa hajali hatari zinazoweza kusababishwa na ngono zembe.

" Wanawake wa Gokwe wanataka pesa, pesa na pesa na pesa zaidi, haijalishi una sura ya aina gani , uwe mchafu au mtanashati ili mradi uwe na pesa utapata mwanamke wa kulala nae. Kwangu mimi huwa sisiti kuwafurahisha pale wanaponipenda.

"hebu angalia kama kuna mchimbaji wa madini hapa ambaye ni mtanashati, lakini bado wanawake wanawafuata, ni kwasababu ya pesa ,"alisema.Makaka mapacha Tafadzwanashe na Tapiwanashe Fichani ni vijana wa Zimbabwe wanaojivunia kuwa Waafrika

Tafadzwa aliliambia gazeti kwamba ameacha kutumia kinga wakati anapofanya ngono.

"Hakuna cha kuogopa tena. Ni mbwa anakula mbwa. Hayo ndio maisha ya wachimbaji wa madini, na sio siri kwamba wengi wao wanakufa kutokana na virusi vya HIV na Ukimwi.

" Niliacha kuvaa mipira ya kinga(kondomu) na sasa ninawalenga wanawake ambao pia wanatumia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (anti-retroviral therapy)," alisema Tafadzwa.

Licha ya yote hayo anasema kuwa anajiangalia kama "mwanamme aliyeoa."

" Nimeoa na na tuna watoto watatu. Mmoja wao jina lake anaitwa Zimbabwe. Nina watoto sita kwa ujumla.

" Watoto wengine watatu nimewazaa na wanawake watatu tofauti ambao waliamua kuniacha. Kwa hiyo kwa sasa ninaishi na mwanamke mmoja baada ya wengine wawili kuniacha kwasababu wasingeweza kuvumilia tabia yangu ya kulala na wanawake tofauti ," Alisema Tafadzwa bila kujali.

Mnamo mwaka 2006 Tafadzwa na pacha yake anayeitwa Tapiwa walivutia umati wa watu baada ya kuondoka nyumbani kwa baba yao na kuamua kuishi mitaani huku wakivaa nguo za ngozi.

Tafadzwanashe na Tapiwanashe Fichani ni vijana wa Zimbabwe wanaojivunia kuwa Waafrika. 

Mnamo mwezi wa Januari 2006 makaka hao walikamatwa na maafisa wa polisi kwa kuvaa mavazi vipande vidogo vya ngozi vilivyoficha tu sehemu zao za siri na kutembea katika maduka makubwa mjini Harare

Awali mapacha hao pia walitiwa nguvuni baada ya kusema kuwa walipokea wito wa Mungu uliowataka waache kuvaa nguo za kimagharibi walipokuwa wakiishi nchini Uingereza.

Makaka hao walisema kuwa watu wanaokosoa uamuzi wao wa kuvaa ngozi wamepumbazwa na utamaduni wa magharibi kwani wao wanarejea kufuata mambo yalivyokuwa kabla ya kuja kwa wazungu Afrika.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527