TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA


Kocha wa Derby County Frank Lampard anaelekea kuteuliwa kuwa meneja wa Chelsea baada ya Maurizio Sarri kukataa ombi la kubakia kikosini. Lampard anamtaka mchezaji mwenzake wa zamani katika klabu hiyo, Didier Drogba awe mmoja wa wasaidizi wake , lakini si John Terry.

Mchezaji wa Manchester United na timu ya taifa yaUfaransa Paul Pogba, 26, anasisitiza kuwa anataka kuondoka United na kuelekea Real Madrid. (Marca)

Crystal Palace imemthamanisha kwa kiwango cha pauni milioni 50 mchezaji wa safu ya Ulinzi ya kikosi cha England cha vijana chini ya miaka 21 - Aaron Wan-Bissaka, ambaye angependa kuhamia Manchester United, lakini hajaonyesha msukumo wa kuondoka katika kikosi cha Palace. (Sky Sports)Aaron Wan-Bissaka, ambaye angependa kuhamia Manchester United, hajaonyesha msukumo wa kuondoka katika kikosi cha Eagles

Tottenham wameachana na mpango wa kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Lisbon, Bruno Fernandes, mwenye miaka 24, ambaye pia amekuwa akihusishwa na uhamisho kuelekea Manchester United. (Mail)

Manchester United wanaamini wanaweza kushinda kinyang'anyiro cha kumsainisha mkataba mlinzi Harry Maguire kwasababu ya kusitasita kwa Manchester City kulipa pauni milioni 80 za ziada kwa ajili ya kumchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 26. (Mail)

Kiungo wa kati wa Chelsea Mbrazil Willian, mwenye umri wa miaka 30, anakaribia kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kusalia katika uga wa Stamford Bridge. (Sun)

Manchester United wako tayari kumuongezea pesa kipa David de Gea, mwenye umri wa miaka 28, kwa azma ya kumshawishi aendelee kubakia katika uga wa Old Trafford baada ya Juni 2020. (ESPN)Manchester United watamtaka De Gea abaki kikosini hata kama ni kutoa pesa za ziada

Ajax watataka kitita cha pauni milioni 30 tu kwa ajili ya kumuachia winga wao raia wa Morocco Hakim Ziyech. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa akihusishwa na tetesi za kutakiwa na vilabu vya Liverpool na Arsenal. (Mirror)

Manchester United wanataka sana kusaini mkataba na mchezaji wa kimataifa wa Argentina Giovani Lo Celso, mwenye umri wa miaka 23, lakini Real Betis wameweka dau la pauni milioni 67 kwa kiungo wao wa huyo ambaye pia amekuwa akihusishwa na klabu ya Tottenham. (inews)

Liverpool wamekwishaonesha nia ya kumtaka winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe, 24 ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Lille. (Le10 Sport, via Daily Express)Arsenal hawatakubali Pierre-Emerick Aubameyang achukuliwe na timu nyingine

Mshambuliaji wa Fulham Mserbia Aleksandar Mitrovic, ambaye amekuwa akihusishwa na West Ham, anakaribia kuhamia Real Betis. (Star)

Arsenal wanapanga kuzungumza na mshambuliaji kutoka Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa miaka 29, ili kumpatia mkataba mkubwa kwa lengo la kuipiku klabu kadhaa za Ligi ya Uchina zinazotaka kumchukua. (Mirror)

Leeds watakataa ofa yoyote kutoka Tottenham ya kumchukua Jack Clarke, 18, anayecheza safu ya ushambuliaji na pia kutoka Aston Villa ofa ya kumchukua kiungo Kalvin Phillips mwenye umri wa miaka 23 . (Star)Manchester United wanataka kusaini mkataba na Mchezaji wa kimataifa wa Argentina Giovani Lo Celso

Kaka yake na wakala wa mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Gonzalo Higuain ameonekana kumaliza uvumi wa kumuhusisha mchezaji huyo wa kuhamia klabu ya AS Roma kwa usema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anataka kumalizia maisha yake ya soka na Juventus. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Chelsea Mbrazil Willian, mwenye umri wa miaka 30, anakaribia kabisa kusaini mikataba miwili ya kubakia katika Stamford Bridge

Meneja mpya wa Roma Paulo Fonseca anaangalia uwezekano wa dau kwa ajili ya kumnasa kiungo wa kati wa Manchester United na raia wa Brazil, Fred, mwenye umri wa miaka 26. (Metro)

Mlinzi wa England Kyle Walker yuko tayari kusaini mkataba wa miaka miwili zaidi katika klabu ya Manchester City. (Manchester Evening News)Mlinzi wa England Kyle Walker yuko tayari kusaini mkataba wa miaka na klabu ya Manchester City.

Manchester United wanaimani kuwa Sean Longstaff anataka kuhamia Old Trafford - licha ya kwamba kiungo huyo kueleza wazi kuwa moyo wake ungali na klabu ya Newcastle.

Brighton wako katika mazungumzo na Genk juu ya mkataba na nahodha wa kikosi cha Ubelgiji na winga Leandro Trossard, mwenye umri wa miaka 24. (Sky Sports) Ni wazi gonzalo higuain hatahamia Roma

Kiungo wa kati wa River Plate Santiago Sosa, mwenye umri wa miaka 20, amehusishwa na uhamisho wa pauni milioni 13 kuelekea Everton, na inasemekana anaweza kupata pasipoti ya EU kutokana na asili yake ya Ulaya , ambayo inaweza kumuongezea bahati yake ya kuhamia katika Primia Ligi msimu ujao.(Liverpool Echo)

SOURCE.BBC SWAHILI.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post