JAMAA AFURAHIA KUFANYA KAZI NA MAITI ...ADAI HAWASUMBUI KABISA!!

Kwa wengi, maiti huogofya sana na ni wachache pekee ambao huwa na ukakamavu wa kuingia kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti. 


Wengi huteta kuwa huathirika na ndoto mbaya wakati wowote wakikutana na maiti. Lakini 

Basil Enatu ambaye hupenda kufanya kazi na maiti. Ni muhudumu wa hifadhi ya maiti nchini Uganda anasema miili ya waliofariki ndio marafiki wake wakubwa.

 Enatu, mwenye miaka 57, ni baba wa watoto kumi na wawili na amekuwa akifanya kazi kama mhifadhi wa maiti kwa takriban miaka 32 katika hospitali ya Soroti nchini Uganda. 

Akiongea na gazeti la Daily Monitor, mzee Enatu anasema huwa ni raha sana kufanya kazi na maiti kwani hawasumbui. 

“Napenda kufanya kazi na waliofariki kwani maiti hawasumbua,” aliambia Daily Monitor mnamo Juni 1,2019. 

Enatu alisema lake ni kuwaosha na kuwavisha maiti na wakati mwingine madaktari pia humtaka awasaidie kuvikata vipande vya mwili wakati wa upasuaji wakati mwili unafanyiwa uchunguzi. 

 Licha kuipenda kazi yake, mzee alisema ina changamoto kwani wengi hukataa hata kumsalimu wakihofia mikono yake. 

“Nimegundua wakati nilipokuwa nashiriki tembo ya pale mtaani, wenzangu hawakutaka kushiriki pamoja nami. Wauzaji vile vile walikuwa wakiosha chombo nilichokitumia kwa maji moto tofauti na wengine,” Enatu alisema.

 Kisa hicho ni sawia na cha Jane Mumbi aliyekuwa akifanya kazi ya kuhifadhi maiti katika chumba cha City. Mumbi alisema hupata raha sana kuhudumia maiti.
Chanzo - Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527