KOCHA STARS AFANYA MABADILIKO KATIKA KIKOSI CHAKE




Kocha mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike amefanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi chake siku chache kabla ya michuano ya AFCON 2019 kuanza nchini Misri.

Amunike amelazimika kumrejesha kikosini mlinzi wa kati wa klabu ya soka ya Azam FC  David Mwantika kuziba na nafasi ya beki mwingine wa Azam FC Aggrey Morris.

Aggrey Morris alipata majeraha katika mchezo wa kirafiki wa Taifa Stars dhidi ya Misri uliopigwa Alhamis Juni 13, 2019 kwenye uwanja wa Borg El Arab jijini Cairo.

Mchezo huo ulimalizika kwa Tanzania kukubali kichapo cha goli 1-0 ambalo lilifungwa Ahmed Elmohamady dakika ya 64. 

Morris aliumia dakika ya 74 na nafasi yake kuchukuliwa na Ally Mtoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527