Kigogo Mstaafu wa Jeshi la Polisi Afariki Kwa Kujinyonga | MALUNDE 1 BLOG

Monday, June 10, 2019

Kigogo Mstaafu wa Jeshi la Polisi Afariki Kwa Kujinyonga

  Malunde       Monday, June 10, 2019
Mkuu wa Mafunzo na Mapambo wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Dar es Salaam, Azizi Juma, anadaiwa kufariki dunia kwa kujinyonga.

Azizi ambaye aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, alikutwa ameshafariki dunia akiwa amening'inia katika mti wa mlimau uliopo nyumbani kwake eneo la Kijichi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Zanzibar, Muhammed Hassan Haji, alisema chanzo cha kifo hicho hakijajulikana.

“Alikutwa amefariki dunia akiwa ananing'inia katika kitanzi kilichofungwa katika mti wa mlimau uliopo nyumbani kwake Kijichi,” alisema.

Alisema kifo chake ni pigo na pengo kubwa kwa Jeshi la Polisi.

Aliitaka familia ya marehemu kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Juma alizaliwa mwaka 1960 huko Michakaeni kijijini kwao kisiwani Pemba. Alizikwa jana jioni katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post