Marekani yaipatia Uturuki onyo la mwisho la ununuzi wa silaha za Urusi

Uturuki imepewa ilani ya hadi mwisho wa mwezi Julai kuchagua kati ya kununua ndege za kivita za Marekani na makombora ya Urusi.

Kaimu waziri wa ulinzi wa Marekani Patrick Shanahan ametoa ilani hiyo katika waraka aliyomwandikia mwenzake wa Uturuki, Hulusi Akar.

Amesema Uturuki, haiwezi kumiliki ndege ya kisasa ya kivita chapa F-35 kutoka Marekani na makombora S-400 kutoka Urusi.

Washirika hao wawili wa muungano wa kujihami kwa mataifa ya Magharibi Nato, wamekuwa wakizozana kwa miezi kadhaa sasa kuhusiana na makombora ya S-400.

Marekani inahoji kuwa silaha hiyo ya Urusi haiambatani na mwongozo wa uundaji silaha ya ulinzi uliyotolewa na Nato na kwamba ni tishio kwa usalama na kuitaka Uturuki kununua ndege yake ya kivita badala ya makombora ''hatari'' ya Urusi.

Uturuki ambayo imekuwa ikijikakamua kuimarisha ulinzi wake kwa kutumia sera huru, imeagiza ndege 100 za kivita aina ya F-35 kutoka Marekani, na pia imewekeza katika mpango wa F-35, huku kampuni zake zikitengeneza vipuri 937 ya sehemu ya ndege hizo.

Suala hili linaonekana kuwa msumari moto kwa mataifa yote mawili ya Uturuki na Marekani.

Akizungumza katika kongamano la kila mwaka la Usalama Duniani, linalofahamikakama Globsec Security Forum mjini Bratislava, Slovakia, Kamanda mkuu mpya wa Nato, Generali Tod Wolters, aliisema "hatuna haja ya kushirikiana katika uwezo wetu wa F-35 na Urusi".

Hii ni wazi kuwa, Pentagon inaamini ikiwa Uturuki itaruhusiwa kununua ndege yake ya kisasa ya kivita chap F-35 na pamoja na mtambo wa kisasa wa kuzuia makombora ya S-400 mafundi wa Urusi wataweza kufikia mitambo ya ndege hiyo hali ambayo itawaweka marubani wa Marekani katika hali ya hatari.

Vikosi vya Marekanai, Uturuki na Urusi tayari vinafanya kazi katika eneo la kaskazi ni mwa Syria.

Lakini mwanadiplomasia wa Uturuki wa ngazi ya juu -ambaye hakutaka jina lake litajwe - ameniambia kuwa Washington ilipinga mpango wa Uturuki kununua mtambo huo wa ulinzi kutoka Urusi baada yapande hizo mbili kutia saini mkataba wa makubaliano.

Saa, anasema,Uturuki haiwezi kujiondoa katika mkataba huo hata kama ingelitaka kuchukua hatua hiyo . Uturuki ikitia saini mkataba, alisema, inaheshimu mkataba huo.

Bw. Shanahan alisma katika barua yake kuwa Marekani "imesikitika" kufahamu kuwa maafisa wa Uturuki wametumwa Urusi kupewa mafunzo ya kuendesha mtambo wa S-400.

"Uturuki haitapokea ndege za F-35 ikiwa atanunua S-400," aliandika . "Bado mna nafasi ya kuamua ikiwa mtabadilisha mawazo kuhusu ununuzi wa S-400."

"Hatutaki F-35 ikaribiane na na makombora ya S-400 kwa muda kwasababu hawana ufahamu wa kina kuhusu vifaa vilivyotumiwa kuunda silaha hiyo," Katibu wa kudumu wa wizara ya Ulinzi Ellen Lord aliwaambia wanahabari.

Ndeg enne za kwanza za F-35 ambazo zilikuwa ziwasilishwe kwa Uturuki bado hazijaondoka rasmi Marekani ili kwawezesha marubani wa Uturuki kuanza kujifunza nazo nchini humo.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema siku ya Jumanne kuw ataifa lake ''limejitolea" kuendelea mbele na utekelezaji wa mkataba wa ununuzi wa makombora ya S-400.

"Kwa bahati mbaya hatukupokea mapendekezo yoyote kutoka Marekani kuhusiana ununuzi wa silaha hii ya S-400 kutoka Urusi,"alisema .

Uturuki ni taifa la pili lililo na wanajeshi wengi katika muungano wa Nato, muungano wa kijeshi uliyo na wanachama 29- ambao ulibuniwa na mataifa ya magharibu ili kujilinda zama za muungano wa Kisovieti.

Uhusiano kati ya Marekani na Urusi ulidorora kwa haraka baada ya Urusi kulimega eneo la Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014.

Madai ya Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 na kuhusika kwake kijeshi nchini Sryria kuliongeza zaidi misukosuko.
 
S-400 ni mfumo wa aina gani?
S-400 au "Triumf" ni moja ya silaha ya hali ya juu duniani inayotoa ulinzi wa ardhini na angani.

S-400 moja ina uwezo wa kuangusha makombora 80 yaliyorushwa umbali wa kilomita 400 kwa wakati mmoja.

Urusi inasema kuwa ina uwezo kuangusha makombora yanayorushwa kutoka kwa ndege zisizo na rubani na makombora ya masafa marefu.

S-400 inafanya vipi kazi?
  1. Ni kifaa kilicho na uwezo wa kutoa taarifa kwa gari maalum inayoelekezwa katika eneo linalolengwa kushambuliwa
  2. Taarifa hizo zinatumwa kwa gari linalosaidia kurusha makombora na kuelekeza makombora angani
  3. Kifaa hiki pia kinasaidia kuelekeza makombora katika eneo maalum
Credit: BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments