RC GAGUTI KUZINDUA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI KAGERA



Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti,anatarajia kizindua kampeni ya msaada wa kisheria kwa wananchi wenye uhitaji ili kutanzua changamoto za kisheria zinazowakabili.

Brigedia Jenerali Gaguti, ametoa kauli hiyo wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake leo Ijumaa Juni 21,2019.

Alisema kampeni hiyo itakuwa ya siku tatu kuanzia tarehe 27 Juni hadi 29 mwaka huu katika viwanja vya Gymukana mjini Bukoba Mkoani huko.

Alisema kampeni hiyo itahusisha watalaamu mbalimbali sanjari na wanasheria wasiopungua 20 ,taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ( TAKUKURU ) Dawati la jinsia ,watu wa ustawi wa jamii pamoja na jeshi la polisi.

"Mimi kama mkuu wa Mkoa nimekuwa nikikutana na wananchi wenye matatizo mbalimbali pamoja na changamoto za kisheria " alisema mkuu wa mkoa huo.

Alisema ofisi yake imeamua kutoa muda maalumu na muafaka wa kufanya kampeni hiyo baada ya kubaini wananchi wengi wanakabiliwa na changamoto za kisheria.

Alisema lengo la kampeni hiyo ni kutanzua changamoto za wanakagera za kisheria hasa maeneo korofi ambayo ni Ardhi,mirathi,unyanyasaji wa kijinsia na kutekeleza familia.

Alisema kwa muda huo wa siku tatu wamepanga kuhudumia watu 2000 na kwa siku watakuwa wanahudumia wananchi 650.

Alisema lengo la kampeni hiyo ni kuwafikia wananchi wote wa Mkoa huo wenye mahitaji lakini wameanza na Wilaya ya Bukoba kwanza.

Alisema muda utakuwa kuanzia saa mbili asubuhi kwa muda huo wa siku tatu .

Na Ashura Jumapili - Bukoba

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527