TANGA UWASA WATEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU KWA VITENDO | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 21, 2019

TANGA UWASA WATEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU KWA VITENDO

  Malunde       Friday, June 21, 2019


 Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo kulia akifanya mazoezi na watumishi wa mamlaka hiyo leo(Ijumaa) jioni

Sehemu ya watumishi wa Tanga Uwasa wakiwa kwenye mazoezi katikati ni Kaimu Afisa Rasilimali Watu wa Tanga Uwasa Theresia Sanga
Mazoezi yakiendelea
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo kulia akiwa na watumishi wenzake wakishiriki mazoezi hayo
Mazoezi yakiendelea kama inavyoonekana

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wameanza utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa kufanya mazoezi siku tatu kwa wiki baada ya muda wa kazi kuisha.

Mazoezi hayo hufanyika Jumanne, Jumatano na Ijumaa ambayo yameonekana kuwa chachu kwa watumishi ambao wamekuwa wakishiriki

Akizungumza mara baada ya kumalizika mazoezi ya leo Kaimu Afisa Rasilimali Watu wa Tanga Uwasa Theresia Sanga alisema wameamua kufanya mazoezi hayo ili kuweza kuimarisha miili yao na kuiweka imara pia husaidia kupunguza msongo wa mawazo.

Alisema pia kupitia mazoezi hayo mbali ya kuimarisha miili yao lakini pia yanajenga umoja na kuweka kujenga ushirikiano kwenye kazi hali inayosaidia kutekeleza majukumu yao vema.

“Lakini pia mazoezi yanaondoa msongo wa mawazo hivyo ni jambo zuri huku akiwahamasisha watumishi kuhakikisha kila wakati wanashiriki kwani yanafaida kubwa kiafya”Alisema

Awali akizungumza Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Dorrah Killo alisema mazoezi hayo ni mazuri kwa sababu yanawapa umoja na kupelekea kupendana ikiwemo kuongeza hari ya uwajibikaji.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post