SERIKALI YAPANDISHA USHURU WA NYWELE ZA BANDIA (MAWIGI)


Serikali imependekeza kupandisha kwa ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za nywele bandia zinazozalishwa nchini na asilimia 25 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje nchi.

Pendekezo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Akizungumza Bungeni jijini Dodoma Waziri Mpango aLIeleza kuwa "napendekeza kutoza ushuru wa asilimia 10 kwenye bidhaa za nywele za bandia, zinazotengenezwa ndani ya nchi na asilimia 25 zazoagizwa kutoka nje ya nchi lengo ni kuongeza mapato ya Serikali."

Mara baada ya Waziri Mpango kuwasilisha pendekezo hilo kwenye bajeti ya Serikali, ukumbi wa Bunge uliripuka kwa kelele kwa Wabunge wakipiga meza zao wakionesha kufurahia pendekezo hilo.

Aidha katika bajeti Waziri mpango alipendekeza kupandishwa tozo leseni ya magari ya pamoja na kuongez a mwaka kutoka miaka 3 hadi miaka 5, kwa mwaka 2018/2019


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527