Picha : KAMBI YA ARIEL 2019 YAFUNGULIWA DAR...VIJANA WANAOISHI NA VVU WAKUMBUSHWA KUTUMIA ARV

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Bi. Asha Mtwangi akifungua kambi ya watoto na vijana kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu inayofanyika jijini Dar es salaam.
***
Watoto na vijana wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya dawa za kupunguza makali ya VVU 'ARV' ili waweze kuboresha afya zao hivyo kutimiza ndoto zao za maisha.


Wito huo umetolewa leo Jumapili Juni 23,2019 na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Bi. Asha Mtwangi alipokuwa akifungua kambi ya watoto na vijana kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu.

Katika kambi hiyo maarufu kama Ariel Camp inayofanyika katika hoteli ya Landmark, Mbezi Beach, Jijini Dar es salaam, Bi. Mtwangi alisema kama ilivyo kwa watoto wasio na VVU, watoto wanaoishi na VVU wana haki zote za kuishi, kupendwa, kusoma na kucheza."Kuwa na maambukizi ya VVU hakuhalalishi kumnyima mtoto haki zake hizo," alisisitiza. 

Aidha Bi. Mtwangi aliipongeza AGPAHI kwa juhudi ambazo imekuwa ikizifanya kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za VVU na UKIMWI kwa watu wanaoishi na VVU. 

"Matarajio yetu na ndoto zetu ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2022 kusiwe na mtoto mwenye UKIMWI," alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa, alisema kambi hiyo ni ya 13 tangu asasi hiyo ianzishe utaratibu wa kukutanisha watoto wanaotoka kwenye klabu za vijana zilizopo katika vituo vya huduma na matunzo vilivyopo kwenye mikoa ambayo AGPAHI inafanya kazi.

"Katika kambi hizi watoto wamekuwa wakibadilishana mawazo, kutiana moyo, kujifunza masuala ya VVU/UKIMWI, kukua, ujinsia na ujasiriamali. Pia wamekuwa wakijengewa ujasiri na kujiamini ili waweze kutimiza ndoto zao," alisema.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Bi. Asha Mtwangi akizungumza wakati akifungua kambi ya watoto na vijana kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za mama na mtoto AGPAHI, Dk. Akwila Temu akifuatiwa na Mkurugenzi wa Taarifa za Takwimu,Utafiti na Ufuatiliaji wa AGPAHI, Dk. Boniphace Idindili. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Bi. Asha Mtwangi akifungua kambi ya watoto na vijana kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu na kuwataka vijana kutokata tamaa katika maisha. 
Vijana wakisikiliza nasaha mbalimbali ukumbini.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Ariel Camp 2019.
Herieth Novati kutoka AGPAHI akisoma historia ya Ariel Camp.
Vijana wakitoa burudani ya wimbo wakati wa ufunguzi wa Ariel Camp.
Vijana kutoka kikundi cha Baba  Watoto wakitoa burudani ya sarakasi.
Muelimisha  rika kutoka mkoa wa Shinyanga akielezea jinsi alivyopata maambukizi kwa kuongezewa damu isiyo salama wakati akiwa mtoto mdogo.
Vijana wakiwa ukumbini.
Burudani ya nyimbo ikiendelea ukumbini.
Viongozi wa AGPAHI wakifuatilia matukio wakati wa ufunguzi wa Ariel Camp.
Mtaalamu wa mambo ya sanaa kutoka kundi la Baba Watoto, Bw. Mkude Kilosa akicheza na vijana wanaoshiriki Ariel Camp 2019.
Picha ya pamoja Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Bi. Asha Mtwangi na Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa,wafanyakazi wa AGPAHI na watoto wao, Baba watoto na washiriki wa Ariel Camp 2019 kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu.
Picha ya pamoja Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Bi. Asha Mtwangi na Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa, washiriki wa Ariel Camp 2019 kutoka mkoa wa Mwanza.
Picha ya pamoja Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Bi. Asha Mtwangi na Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa, washiriki wa Ariel Camp 2019 kutoka mkoa wa Simiyu.
Picha ya pamoja Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Bi. Asha Mtwangi na Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa, washiriki wa Ariel Camp 2019 kutoka mkoa wa Shinyanga.
Picha ya pamoja Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Bi. Asha Mtwangi na Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa, washiriki wa Ariel Camp 2019 kutoka mkoa wa Mara.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527