DR. NDUGULILE ATOA RAI KWA JAMII ZENYE NDOA ZA ASILI KUSAJILI SERIKALINI


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Ikiwa leo Juni 23,2019  ambapo Tanzania imeungana na mataifa mengine Ulimwenguni kuadhimisha siku ya Wajane Duniani,Naibu  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii jinsia ,Wazee  na Watoto Dokta.Faustine Ndugulile  ametoa rai kwa jamii zenye ndoa za Asili kusajili  Serikalini ili kuondoa usumbufu baadaye pindi wanapohitaji kutafuta haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na mirathi. 


Dokta.Ndugulile ametoa rai hiyo leo Juni  23,2019 katika kilele cha siku ya Wajane Duniani ambapo kwa Tanzania yamefanyika katika viwanja vya Nyerere Square  jijini Dodoma. 


Dokta Ndugulile amesema hapa nchini Tanzania hususan vijijini watu wengi hawajui  haki zao   hivyo ni muhimu kusajili ndoa zao za asili katika mamlaka husika za  serikali huku akizitaka Taasisi za serikali zinazohusika na masuala ya mirathi kutoa elimu kwa jamii kuhusu taratibu za Mirathi kwani pamekuwepo kwa baadhi ya ndugu wasio wahusika wamekuwa wakiwageuka walengwa wa mirathi na kujifanya wasimamizi wa miradhi kwa nia mbaya ya kujipatia mali huku walengwa wa Mirathi hiyo wakiachwa wakihangaika. 


Katika hatua nyingine Dokta Ndugulile amesema maandalizi ya Wosia  yanatakiwa kuanza mapema ili kuondoa na kupunguza  migogoro ya mirathi inayojitokeza pindi mwenza mmoja anapofariki. 


Hata hivyo,Dokta Ndugulile amewatia moyo Wajane na kusema kuwa Ujane sio Mwisho wa Maisha na kinachotakiwa ni kutokata tamaa bali ni kufanya kazi za maendeleo na kuinua uchumi kwao.

Siku   Ya   Wajane  Duniani imekuja kutokana na kampeni za mwanasiasa mmoja Muingereza ambae, alifiwa na baba yake akiwa mtoto  nchini India  ambapo   Serikali ya Gabon ilidhamini azimio hilo la Umoja wa Mataifa    na  Inakisiwa kuna takriban wajane millioni 245 duniani na 115millioni wanadhulumiwa wakikabiliwa na ukatili,umasikini na kutengwa na jamii.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post