Picha : UMOJA WA MAKANISA YA KIPENTECOSTE,KIINJILI SHINYANGA WAFANYA MAZOEZI NA KUCHANGIA DAMU SALAMA


Na Marco Maduhu - Malunde1 blog.
Umoja wa makanisa ya Kipentecoste Mkoani Shinyanga wamefanya mazoezi na kuchangia damu salama, ili kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kuimarisha afya za wananchi, pamoja na kuokoa vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi kwa sababu ya kumwaga damu nyingi.


Mazoezi hayo yamefanyika leo Juni 15, 2019 kwenye uwanja wa wamichezo wa Sabasaba, na kuongozwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga, mhe. Jasinta Mboneko, ambayo yalianza kwa matembezi na kukimbia kwa kuzunguka mji wa Shinyanga na kuhitimishwa kwa kuchangia damu salama.


Akizungumza kwenye mazoezi hayo, mwenyekiti wa umoja wa makanisa hayo ya Kipentecoste mkoa wa Shinyanga,Askofu Elias Madoshi, amesema wao kama viongozi wa kidini wameona ni vyema kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi pamoja na kuchangia damu salama.


Amesema juhudi za serikali ya awamu ya tano zinapaswa kuungwa mkono, ambapo wananchi wakiwa na afya mgogoro kamwe hawataweza kufaya shughuli za uzalishaji mali, na hatimaye nchi kushindwa kukua kimaendeleo na kufikia kwenye uchumi wa kati.


“Sisi kama Umoja wa makanisa ya Kipentecoste mkoani Shinyanga CPCT kwa kushirikiana na umoja wa makanisa ya Kiinjili CCT, Tumeamua kuungana na Serikali kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi ili wawe na afya imara, pamoja na kuchagia damu salama ili kuokoa vifo vya mama na mtoto vikonavyo na uzazi kwa kumwaga damu nyingi wakati wa kujifungua”amesema Madoshi.


“Hivyo tunatoa wito kwa wananchi mkoani Shinyanga wajikite kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao pamoja na kujitoa kuchangia damu salama, ambayo itaokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu ikiwamo na kumaliza vifo vya uzazi vitokanavyo na umwagaji damu nyingi,”ameongeza.


Naye mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amepongeza Umoja huo wa makanisa ya Kipentecoste kwa kutoa hamasa ya wananchi kushiriki kufanya mazoezi pamoja na uchagiaji wa damu salama.

Amesema mazoezi hayo yalizinduliwa na makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambayo yatafanyika kila Jumamosi ya pili ya mwisho wa mwezi, na kuwasihi watumishi wa serikali kuwa mfano wa kuigwa kushiriki kwenye mazoezi hayo na siyo kuwa wategeaji, ambapo ataanza kuwa anapitisha daftari la ukaguzi wa majina ya watumishi.


Kwa upande wake mratibu wa Damu salama mkoani Shinyanga,Dkt. Joel Mdale, ametoa shukrani kwa umoja huo wa makanisa ya kipentecoste kwa hamasa hiyo ya uchangiaji wa damu salama, jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba wa damu kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa, na hatimaye kuokoa vifo vya wagonjwa wenye uhitaji wa damu wakiwamo wajawazito.


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiwataka wananchi kuendelea kufanya mazoezi ambayo yatawasidia kuimarisha afya zao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akitoa wito kwa wananchi pia kuwa wawe wanajitokeza kuchangia damu salama, ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu hiyo wakiwemo na akina mama wajawazito na watoto.

Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentecoste mkoani Shinyanga Askofu, Elias Madoshi, akielezea namna walivyohamasika kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya Tano, kwa kufanya mazoezi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuchagia damu salama kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Mratibu wa damu salama mkoani Shinyanga Dkt. Joel Mdale, akielezea namna alivyoguswa na uhamasishaji wa uchangiaji wa damu hiyo salama, ambao utaondoa upungufu wa damu hiyo na kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu hiyo wakiwamo wajawazito.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko katikati mwenye kofia akiongoza mazoezi kwa kutembea kwa miguu pamoja na kukimbia kwa kuzunguka mji wa Shinyanga.

Mazoezi ya matembezi na kukimbia yakiendelea.

Mazoezi yakiendelea.

Mazoezi yakiendelea.

Mazoezi yakiendelea kwenye uwanja wa Sabasaba mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kutembea na kukimbia kwa kuzunguka mji wa Shinyanga.

Mazoezi ya kunyoosha viungo yakiendelea kwa ajili ya kuhitimisha mazoezi na kuanza uchangiaji wa kutoa damu salama.

Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akipima uzito tayari kwa kuchangia damu salama.

Viongozi wa dini kutoka makanisa ya kipentecoste mkoani Shinyanga wakiwa na wananchi pamoja na watumishi wa Serikali kwenye mstari kwa ajili ya kuchangia damu salama kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, akiendelea kuhamasisha wananchi kuchangia damu salama pamoja na kuchukua kadi za uchangiaji wa damu hiyo.

Mratibu wa damu salama mkoani Shinyanga Joeli Mdale akimtoa damu Askofu Josephat Msila kutoka kanisa la Kipentecoste (TMRC) Ndembezi mjini Shinyanga.

Zoezi la uchangiaji damu salama likiendelea.

Zoezi la uchangiaji damu salama likiendelea.

Zoezi la uchangiaji damu salama likiendelea.

Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la (TAG) mkono wa kulia, akimpatia cheti cha Pongezi kwa kazi anazozifanya mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, pamoja na mkuu wa mkoa huo Mhe. Zainab Telack.

Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la (TAG) mkono wa kulia, akimpatia cheti cha Pogezi Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao kwa kazi nzuri anazofanya za kulinda amani mkoani humo.

Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la (TAG) mkono wa kulia, akimpatia cheti cha Pongezi mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Shinyanga (RTO), Antony Gwandu kwa kazi nzuri anayofanya ya kupuguza ajali mkoani humo.

Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la (TAG) mkono wa kushoto, akimkabidhi cheti cha Pongezi mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga (DTO) Emmanuel Palangyo kwa kazi nzuri anayoifanya ya kusimamia usalama barabarani na kupuguza ajali.

Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la (TAG) mkono wa kulia, akikabidhi cheti cha Pongezi kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoani Shinyanga.

Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la (TAG) (kulia) akikabidhi cheti cha pongezi kwa makamu mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) Shabani Alley kwa kazi nzuri inayofanywa na waandishi wa habari mkoani Shinyanga kuhabarisha wananchi.

Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la (TAG) Shinyanga, akiombea amani mkoani Shinyanga katika kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post