BIA YA SERENGETI LITE YATUNUKIWA TUZO YA SUPERBRAND

Mei 7,2019, Dar es Salaam: Bia ya Serengeti Premium Lite imepata tuzo ya Superbrands kwa mwaka 2019/2020 kama ishara ya kutambua ubora wake wa hali ya juu, kuaminika kwake na wateja na uhalisia kwa watumiaji wake.

Ikiwa imepigiwa kura na watu wapatao 1000 nchini kote na kuthibitishwa na baraza la huru la wataalamu wa sekta ya uzalishaji, Serengeti Lite inaingia katika duru za kihistoria kwa tuzo hii ya kifahari ikiwa moja ya ubunifu wa hivi karibuni kabisa uliofanywa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL). Bia mama ya Serengeti Premium Lager nayo ni pia ni mshindi wa tuzo ya Superbrands.

"Kushinda tuzo ya Superbrand ni muhimu zaidi kuliko wakati wowote hasa ukichukulia hali ya uchumi na ushindani katika sekta ya bia kwa ukanda huu unaongezeka kwa kasi kubwa. Hakika, kushinda tuzo hii ni ishara tosha ya juhudi za Serengeti Lite kuendelea kuwa bidhaa muhimu, ya tofauti na ya kuvutia machoni mwa watumiaji, "amesema AnithaRwehumbiza, Meneja Masoko wa SBL katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kampuni leo hii.

Serengeti Lite inayotambulika zaidi kama ‘The only Lite with a Bite’ ikiwa na maana kwamba ya kuwa na ladha murua ilizinduliwa rasmi Mei, 2017 ambapo katika kipindi cha chini ya miaka miwili kwenye soko, Serengeti Lite imejiimarisha na kuwa lite bia inayoongoza hapa nchini.

Aidha, Kinywaji hicho kimekuwa mdhamini mkuu wa ligi kuu ya soka la wanawake Tanzania maarufu kama ‘Tanzania Serengeti Lite Women’s Premier League’ maarufu kama “The League with a Bite” ambayo imeleta mapinduzi makubwa kwenye soka la wanawake hapa nchini.

Kushiriki katika Superbrands ni kwa mwaliko tu, na mwaliko huo hutolewa kwa bidhaa bora zaidi katika soko.

Kila mwaka maelfu ya bidhaa kutoka sekta tofauti zinaamuliwa dhidi ya ya vigezo vitatu vya muhimu vya Superbrand: ubora, kuaminika na utofauti. Kufikia hali ya kutunukiwa hadhi ya Superbrands ina maana hadhi ya bidhaa husika inaongezeka na huwahakikishia watumiaji na wauzaji kuwa wananunua bidhaa iliyobora kabisa.

“Kipaumbele kikubwa kikiwa kwa wateja wetu kwa kila tunachokifanya, kutunikiwa tuzo ya Superbrand ni mafanikio ya kujivunia sana kwa SBL. Ikiwa ipo kwenye baa, klabu za usiku au maduka makubwa, tunataka kuwahakikishia wateja wetu kuhusu lengo letu la kuendelea kuwapa Lite bora zaidi wakati wote,” ameongeza Rwehumbiza. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post