MASAUNI ASEMA POLISI HAWARUHUSIWI KUMPIGA AU KUMTESA MTUHUMIWA


Wizara ya Mambo ya Ndani  imesema hakuna sheria inayomruhusu askari wa Jeshi la Polisi kumpiga au kumtesa mtuhumiwa wa makosa mbalimbali akiwa mikononi mwa polisi au kituoni.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusuf Masauni amesema kanuni za kudumu za utendaji wa Jeshi la Polisi (PGO) zinakataza na kuelekeza utendaji mzuri wa askari  ambapo polisi yeyote anapobainika kufanya vitendo vya kumpiga au kumtesa mtuhumiwa hufikishwa mahakamani.

Masauni alikuwa akijibu swali la msingi la Mbunge Chonga (CUF), Mohamed Juma Khatibu bungeni, leo Mei 10, 2019, aliyetaka kujua ni kwa mazingira gani askari polisi anapaswa au hulazimika kumtesa mtuhumiwa wa makosa mbalimbali wakati akiwa mikononi mwake au kituo cha polisi.

Naibu waziri huyo amesema, "kwa kutumia PGO, askari wanaokiuka na kufanya vitendo hivyo tunachukua hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi au kufikishwa mahakamani."

Masauni ameliambia Bunge kwamba Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20, kifungu cha 11 kinaeleza namna ya ukamataji.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527