TANASHA AKIRI KUCHANGANYWA NA PENZI LA DIAMOND PLATNUMZ


Mpenzi  wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch amesema kuwa, ilibaki kidogo apate uchizi baada ya kutoka na msanii huyo.

Akizungumza na Citizen TV katika Kipindi cha 10 Over 10, Tanasha ambaye pia ni msanii wa muziki na Mtangazaji wa Radio NRG ya nchini humo alisema kuwa alipoanza kuwa na uhusiano na Diamond  yalizuka maneno mabaya kwake ambayo yalitaka kumpa uchizi.

“Mwanzoni maneno hayo nilichukulia kawaida tu. Yakaanza kunifanya kupata msongo wa mawazo, lakini nilikabiliana nayo,” alisema Tanasha.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527