Angalia Picha : MWENGE WA UHURU WATUA KWA KISHINDO MANISPAA YA SHINYANGAMbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga umekimbia jumla ya kilomita 102 na umezindua miradi nane na kuweka mawe ya msingi, yenye jumla ya shilingi Bilioni 1.3 ambapo hakuna hata mradi mmoja uliokutwa na dosari na kukataliwa.


Mwenge huo umekimbizwa leo Mei 11, 2019 katika Manispaa ya Shinyanga na kuzindua, kutembelea pamoja na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo mbalimbali ikiwamo ya Sekta ya afya, elimu, maji na kiuchumi.

Akizungumza wakati akipokea Mwenge huo wa uhuru mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewataka wananchi wa Manispaa ya Shinyanga kuitunza miradi hiyo ya maendele ili iweze kuwa na tija katika kuwatatulia changomoto zinazowakabili.

“Nawaomba wananchi wa manispaa ya Shinyanga muitunze miradi hii na kutoiharibu ili idumu kwa muda mrefu na kuwatatulia changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili ikiwa serikali inatumia gharama nyingi hadi kuikamilisha,”amesema Mboneko.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Mzee Mkongea Ali amewataka watendaji wa serikali wakiwemo wahandisi kuwa wanaisimamia vizuri miradi ya maendeleo ili ipate kudumu kwa muda mrefu na kuondoa kero kwa wananchi.

Amesema huu ni wakati sasa wa watendaji wa serikali ambapo wanapaswa kufanya kazi kwa kujituma, uadilifu, pamoja na kuwa wabunifu.na siyo kusubiri hadi kuanza kusukumwa hali ambayo wataisaidia serikali kufikia kwenye uchumi wa kati.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi wa Manispaa ya Shinyanga kujitokeza kushiriki kwenye uchuguzi wa serikali za mitaa ili kuchagua viongozi ambao watawafaa kuwaongoza na kuwatatulia kero zao.

Aidha Mwenge huo uhuru umezindua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuweka mawe ya msingi ukiwamo ujenzi wa madarasa matano ya shule ya msingi viwandani na ofisi ya walimu, nyumba za polisi na Ofisi ya tarafa ya Ibadakuli.

Miradi mingine ni mradi wa maji Masekelo,zahanati ya Mwawaza, huku ya watu binafsi ikiwa ni ya ufugaji wa samaki uliopo kata ya Kizumbi ambao unamilikiwa na Mwananchi Garage pamoja mradi wa Petrol Station.

Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu (2019) inasema ,'Maji ni uhai tutunze vyanzo vyake ,wananchi washiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa'.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko mkono wa kushoto akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha (kulia), tayari kwa kuukimbiza kwenye Manispaa ya Shinyanga Kilomita 102 pamoja na kuzindua, kuona na kuweka mawe ya msingi miradi nane ya maendeleo yenye jumla ya Shilingi Bilioni 1.3. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto) akimpokea mkimbiza Mwenge wa uhuru kitaifa  Mzee Mkongea Ali tayari kwa kwenda kukagua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo.

Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mapokezi ya Mwenge huo wa Uhuru.

Mwenge wa uhuru ukianza kukimbizwa tayari kwa uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Manispaa ya Shinyanga pamoja na kuweka mawe ya msingi.

Mwenge wa uhuru ukianza na uzinduzi wa mradi wa ufugaji Samaki katika kata ya Kizumbi unaomilikiwa na Mwananchi Garage.Pichani ni Meneja mradi huo wa samaki,Hanry Kimario akisoma risala kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 120.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Mzee Mkongea Ali akikagua mradi wa ufugaji samaki kabla ya kuuzindua rasmi.

Ukaguzi wa mradi wa samaki ukiendelea.

Samaki wakionekana.

Meneja mradi wa ufugaji Samaki Hanry Kimario mwenye tisheti ya bluu, akitoa maelezo namna wanavyoendesha ufugaji wa samaki hao pamoja na namna ya kuwahudumia.

Ukaguzi wa mabwawa ya samaki ukiendelea.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa  Mzee Mkongea Ali, akiweka vifaranga vya samaki kwenye mradi huo kama ishara ya kuuzindua rasmi.

Uwekaji wa vifaranga vya samaki ukiendelea.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa  Mzee Mkongea Ali, akipanda mti kwenye mradi huo wa kufuga samaki.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa  Mzee Mkongea Ali, akiuzindua rasmi mradi huo wa kufuga samaki mara baada ya kulizika nao.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa  Mzee Mkongea Ali, akikagua ujenzi wa madarasa matano na ofisi katika shule ya msingi viwandani Manispaa ya Shinyanga.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa  Mzee Mkongea Ali,akizungumza huku akiwa ameshika makablasha mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa madarasa matano na ofisa katika shule hiyo ya viwandani manispaa ya Shinyanga na kuweka jiwe la msingi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa  Mzee Mkongea Ali, akiweka jiwe la msingi na kuzindua mradi kwenye kituo cha mafuta, kinachomilikiwa na mtu binafsi ambacho kimegharimu shilingi milioni 700.

Wananchi wakishuhudia uzinduzi wa mradi wa kituo cha mafuta.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa  Mzee Mkongea Ali, akiwataka wamiliki wa vituo vya kuuzia mafuta wafanye biashara zao kwa uaminifu na kuacha uchakachuaji wa mafuta hayo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2019  Mzee Mkongea Ali, akikagua nyaraka mbalimbali kwenye ujenzi wa ofisi ya tarafa ya Ibadakuli manispaa ya Shinyanga kabla ya kuweka jiwe la msingi.

Wakimbiza Mwenge wa uhuru Kitaifa wakiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko na wataalamu wa manispaa ya Shinyanga wakiendelea na ukaguzi wa jengo la ofisi ya tarafa ya Ibadakuli.

Mmoja wa viongozi wakimbiza Mwenge kitaifa akivunja tofali kwenye Tanki la maji taka katika ofisi ya taarafa hiyo ya Ibadakuli ili kujiridhisha kama yana kiwango.

Muonekano wa Jengo la tarafa ya ofisi ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga, ambalo limegharimu shilingi milioni 25.4.


Kaimu Meneja ufundi mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Shuwasa manispaa ya Shinyanga Yusuf Katopola akisoma risala ya mradi wa maji uliopo kata ya Masekelo manispaa ya Shinyanga kabla ya kuzinduliwa na Mwenge wa uhuru.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa  Mzee Mkongea Ali, akikagua mradi wa maji wa SHUWASA kabla ya kuweka jiwe la msingi na kuuzindua rasmi ambao umegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 179.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa  Mzee Mkongea Ali, akimtwisha mmoja wa wanawake ambao wamehudhulia kwenye uzinduzi huo wa mradi wa maji SHUWASA.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa  Mzee Mkongea Ali, akifungua rasmi mradi huo wa maji wa SHUWASA ambao upo kata ya Masekelo, kwa lengo na kuwaondolea adha wakazi wa eneo hilo la kutumia maji machafu.

Wananchi wakishuhudia uzinduzi wa mradi huo wa maji na Mwenge wa uhuru.

Mwenyekiti wa ujenzi wa nyumba 10 za askari polisi mkoani Shinyanga Inspekat Cosmas Taligula akisoma taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo kabla ya kukaguliwa na kuwekewa jiwe la msingi na Mwenge wa uhuru, ambazo zimegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 225.

Wakimbiza Mwenge wa uhuru kitafia mwaka 2019 wakikagua ujenzi wa nyumba za Askari Polisi Shinyanga Mjini.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa  Mzee Mkongea Ali, akipanda mti mbele ya nyumba za askari polisi Shinyanga Mjini.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa  Mzee Mkongea Ali, akiweka jiwe la msingi kwenye makazi ya nyumba za askari polisi Shinyanga Mjini.

Muonekano wa nyumba 10 za makazi ya askari polisi Shinyanga Mjini.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa  Mzee Mkongea Ali, akiwataka vijana wa kikundi cha bodaboda, ambao wamepata mikopo ya bodaboda saba na bajaji moja wazingatie sheria za usalama barabarani pamoja na kuwa wanavaa kofia ngumu.

Bodaboda saba na Bajaji moja ambazo wamekopeshwa vijana kupitia asilimia 10 za mapato ya ndani ya halmashauri ya manispaa ya Shinyanga zilizogharimu shilingi Milioni 24.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa  Mzee Mkongea Ali akikagua risala ya utii ya manispaa ya Shinyanga.

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mwenge huo wa uhuru.

Baadhi ya watumishi wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Mwenge wa uhuru.

Burudani zikitolewa kwenye mbio hizo za Mwenge wa uhuru manispaa ya Shinyanga.

Burudani zikitolewa kwenye Mbio hizo za Mwenge wa uhuru manispaa ya Shinyanga.

Picha zote na Marco Maduhu-Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post