MAKAMU WA RAIS BUNGE LA AFRIKA AMLILIA DR. REGINALD MENGI


Mhe. Stephen Masele

Makamu wa rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi kilichotokea huko Dubai Falme za Kiarabu.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter,Mheshimiwa Masele ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) ameandika :


"Nimepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo cha mzee wetu Reginald Abraham Mengi. Mzee Mengi atakumbukwa daima kwa mchango wake wa maendeleo kwa taifa letu. Naungana na watanzania wenzangu kumuombea na kuwapa pole ndugu na marafiki wote.Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani.Amen"- Stephen Masele.R.I.P Dr. Reginald Mengi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post