MAKONDA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIWA NA MAFURIKO JIJINI DAR


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana amefanya ziara ya ukaguzi wa athari za mafuriko ambapo amesema serikali imeanza kukarabati miundombinu iliyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha ikiwemo madaraja, barabara, mito na mifereji.



Akizungumza wakati wa ukaguzi huo Makonda,  amesema miongoni mwa maeneo yanayoboreshwa na pesa ipo tayari ni mto msimbazi wenye urefu wa km 19 na eneo la Jangwani ambalo maboresho yake yatagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 200 ikiwa ni mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Aidha Makonda amesema hadi sasa jumla ya watu wawili wamefariki kutokana na mvua ambapo amewapa pole wananchi waliokumbwa na athari za mafuriko ikiwemo wale ambao mali zao zimeharibiwa na wengine kulazimika kuyahama makazi yao.

Katika hatua nyingie Makonda amewataka wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Dengue kwa kuhakikisha wanatokomeza mazalia ya mbu na kuhakikisha wanawahi vituo vya afya pindi wanapoona dalili za homa.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527