MCHOMELEA VYUMA ATOA USHAHIDI MAHAKAMANI KESI YA VIGOGO CHADEMA


Shahidi wa pili katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa CHADEMA, Shaban Abdallah (19), amedai alimuona Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akiwahamasisha wananchi kuendelea kuandamana.


Shahidi huyo ambae ni Mchomelea Vyuma anayeishi Kinondoni Moscow ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati akitoa ushahidi wake.

Shahidi Abdallah amedai Februari 16, 2018 majira ya saa 11 jioni alikuwa dukani eneo la Kinondoni Mkwajuni alisikia zogo likisogea karibu na eneo hilo ambapo aliona waandamanaji wakiwa katika hali ya shari wakiimba ‘Hatupoi mpaka mmoja afe watatuua’ ambapo alijua ni watu wa CHADEMA kutokana na mavazi yao na bendera.


Ameeleza kuwa wakati wakiendelea kuwaangalia waandamanaji hao waliona gari la polisi likiwa nyuma yao likiwatangazia watawawanyike, lakini waliendelea kulisogelea na kuanza kurusha chupa za maji na mawe..Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 15, 2019 ambapo washitakiwa wengine ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu,Mbunge wa Kibamba,John Mnyika,Mbunge wa Kawe,Halima Mdee,Mbunge wa Tarime Mjini,Esther Matiko,Mbunge wa Iringa Mjini,Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Vijijini,John Heche.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post