Breaking News ; RAIS MAGUFULI AMTUMBUA MKUU WA MKOA WA KATAVI AMOS MAKALLA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli amempandisha hadhi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuanzia leo, Mei 14,2019.

Uteuzi huo wa Homera umetokana na uamuzi wa wa Rais kumpumzisha aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Amos Makala na kwamba uteuzi wa mkuu wa Wilaya ya Tunduru utafanywa baadaye.

Homera aliteuliwa kuiongoza Wilaya ya Tunduru mwaka 2016 na mpaka anapandishwa wadhfa huu, alikuwa hajahamishwa eneo hilo la kazi.

Kabla ya kupelekwa Katavi Julai mwaka jana, Makalla alikuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya alikodumu tangu mwaka 2016 Dkt. Magufuli alipofanya uteuzi wa kwanza wa wakuu wa mikoa na wilaya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527