MAHAKAMA YAAMURU KURA KUHESABIWA UPYA MALAWI


Mahakama nchini Malawi imeiamuru tume ya uchaguzi kutotangaza matokeo ya uchaguzi wa rais wa Mei 21 kufuatia malalamiko ya wizi wa kura yaliyotolewa na upinzani. 

Katika amri hiyo, Mahakama Kuu ilitaka kusitishwa utangazaji wa matokeo ya kura ya rais na kuelekeza kuhesabiwa upya kwa kura za theluthi ya maeneo yaliyoshiriki uchaguzi. 

Tume ya uchaguzi nchini humo ilisimamisha kutangaza matokeo hayo baada ya kupokea malalamiko 147 kutoka kwa baadhi ya vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi huo wa Jumanne iliyopita. 

Chama kikuu cha upinzani cha Malawi Congress (MCP) kinachoongozwa na Lazarus Chakwera, kiliwasilisha malalamiko mahakamani juu ya kile ilichodai kuwa makosa yaliyojitokeza katika wilaya 10 kati ya 28 nchini humo. 

Ujumbe wa Waangalizi wa Umoja wa Ulaya uliueleza uchaguzi huo kuwa ulisimamiwa vizuri, ulikuwa na uwazi pamoja na ushindani mkali.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post