IRAN YAAPA KUJILINDA KWA NGUVU ZOTE DHIDI YA UCHOKOZI


Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran, Mohammad Javad Zarif, amesema nchi yake itajilinda kwa nguvu zote dhidi ya uchokozi wa kijeshi na kiuchumi, huku akizitolea wito nchi za Ulaya kuchukua hatua zaidi kuyanusuru makubaliano ya nyuklia waliyotia saini. 

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi habari mjini Baghdad, Iraq, hivi leo, Zarif amesema nchi yake inataka kujenga mahusiano ya usawa na jirani zake wa eneo la Ghuba na imekwishapendekeza kutiwa saini mkataba wa kuepuka uchokozi.

 Wakati huo huo, Rais Hassan Rouhani wa Iran ameashiria kuwa Iran inaweza kuitisha kura ya maoni kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo kufuatia kuongezeka mvutano kati yake na Marekani. 

Rouhani amesema amewahi kupendekeza suala hilo kwa Kiongozi  Mkuu Ayotallah Ali Khamenei mwaka 2004 alipokua mjumbe mwandamizi kwenye mazungumzo ya nyuklia. 

Kura hiyo ya maoni itaipa serikali ya Iran uhalali wa kisiasa iwapo itaamua kuongeza urutubishaji wa madini ya urani unaozuiwa chini ya makubaliano ya 2015 na mataifa yenye nguvu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post