POLISI WASEMA ASKOFU GWAJIMA SI MTUHUMIWA WA VIDEO CHAFU…WANANCHI WAONYWA KUISAMBAZA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, May 8, 2019

POLISI WASEMA ASKOFU GWAJIMA SI MTUHUMIWA WA VIDEO CHAFU…WANANCHI WAONYWA KUISAMBAZA

  Malunde       Wednesday, May 8, 2019

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa leo Jumatano April 8, 2019 amezungumzia tena sakata la video ya ngono inayodaiwa kuwa ya Askofu Josephat Gwajima na kusema kuwa Askofu huyo kwa sasa sio mtuhumiwa, bali ni muhanga aliyeathiriwa na tukio hilo.

Amesema  kwa kushirikiana na mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai (DCI), Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa video  hiyo ya ngono inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

"Jeshi la Polisi Kanda Maalumu limeanza uchunguzi wa video hiyo mara moja na linapenda kuwapa taarifa wananchi (kuwa) Gwajima siyo mtuhumiwa, ni muathirika wa tukio hilo kwani tukio hilo linaweza kufanywa na mtu yeyote kwa nia ya kutaka kuharibu heshima yake kwa jamii na waumini," amesema Mambosasa.

Mambosasa ametoa wito kwa wananchi kuacha kusambaza video hiyo kwa maelezo kuwa ni kosa la jinai na kuwataka waumini wa kanisa hilo kuwa watulivu kwani uchunguzi unaendelea ili kubaini aliyeisambaza na lengo la kufanya hivyo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post